TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

Kifo ni fundisho kwako pia unayejiona mwerevu sio lazima uwe mtangazaji. Maandiko yanasema, kwa uzai uleule unaotumia kupimia wenzio, nawe utapimiwa. Duniani tunaingia mmoja mmoja, na tunatoka mmoja mmoja. Hatujui muda wa kuingia wala kutoka. Kila nafsi ipambane na nafsi yake. Ruge na Kibs walifanya kivyao nawe unafanya kivyako. Kama yako yakujifunza toka kwa waliotangalia vyema, kama hakuna nayo ni vyema. Binafsi Ruge amenifundisha kutoa sio lazima iwe pesa, na sio lazima uite vyombo vya habari vistream live. Ufanye kwa nafsi yako, sio kuonyesha jamii kuwa unafanya. Ruge amenifundisha pia kuwa sio watanzania wote wana roho mbaya ya uchoyo, ubinafsi na uzandiki.
 
Mkuu wa mkoa anatoa taharifa za vifo siku hizi

Ndo tulipofika mkuu. Mwananchi wa kawaida ukitoa taarifa utashtakiwa maana wewe siyo mamlaka.
Kuna jamaa yangu alipata ajali ya gari usiku akafa pale pale. Mwanzoni kabla hajafa tulikuwa tunahaha kwenda kuokoa maisha yake lakini kabla hatujaondoka tukapigiwa simu kuwa amesharest in peace. Kwa sababu ni ajali ya gari, nikawaambia wenzangu twendeni polisi kutoa taarifa. Tulipofika tukatoa maelezo, ila tuliposema kuwa kuna mtu amefariki eneo la tukio walituchenjia mpaka tukafuta kauli. Eti mpaka mamlaka husika ithibitishe kuwa kweli kafa.... Basi bwana ikabidi tuwasihi twendeni eneo la tukio ili wahakikishe.

Mambo ni mengi na mengi yamekuwa mambo
 
Kifo kinathibitishwa na daktari, kwahivyo kama daktari hakusema basi mtu mwingine hapaswi kutoa taarifa bila uthibitisho.....
Ivo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…