Mtangazaji wa TV3 Gwamaka Francis aliyetangazwa kupotea siku kadhaa nyuma apatikana kwa shangazi yake Kitunda

Mtangazaji wa TV3 Gwamaka Francis aliyetangazwa kupotea siku kadhaa nyuma apatikana kwa shangazi yake Kitunda

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya kupatikana kwa Mtangazaji wa TV 3, Gwamaka Francis Gehas maarufu kama 'Boiboi Mkali' mkazi wa Mbezi Beach Africana, Dar es Salaam, aliyedaiwa kupotea tarehe 3 Januari, 2025 amepatikana akiwa kwa shangazi yake Kitunda, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime iliyotolewa jana Januari 5, 2025 imebainisha kuwa baada ya ufuatiliaji ulioanza kwa kukusanya ushahidi na taarifa kutoka kwa watu mbalimbali, jana majira ya saa kumi na moja jioni, Jeshi hilo lilipokea taarifa kuwa Gwamaka yupo Kitunda nyumbani kwa shangazi yake.

tv3.png

Aidha, Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kupata maelezo yake ili kujua uhalisia wa tukio la kutokuonekana kwake na baadaye kuonekana akiwa kwa shangazi yake Kitunda.

Ikumbukwe kuwa kituo cha TV3 siku ya tarehe 4 kilitangaza kupotea kwa mtangazaji wa TV3 Gwamaka Francis maarufu kama Boi Mkali ambapo mtangazaji huyo alipotea kuanzia saa 3 asubuhi ya Januari 3 na kwenda kusikojulikana.

TV31.png
 
Back
Top Bottom