Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mtangazaji wa kipindi cha Goodmoring cha Wasafi FM Gerald Hando ametaka au kushauri mtandao wa TikTok Tanzania ufungiwe akidai unaleta matatizo ya afya ya akili kwa vijana wengi zaidi.
Amesema vijana sasa wakilala wakiamka wanawaza wapata bando ili waingie TikTok wafanye mambo yao na akikosa bando yupo tayari apoteze heshima na utu wake ili apate bando tu.
Hii imekaaje jamani mbona kuna harakati nyingine hazina afya kabisa. Kama kuna changamoto ni bora wakasema ziweke sawa kuliko kufikia hatua ya kutaka kufungia mtandao husuki.
Maana kwa sasa mitandao hii ya kijamii kiukweli kabisa imekuwa sehemu ya ajira kwa vijana wengi sana so akitokea mtu anaeta hoja kama hii bila shaka vijana wanaweza wakampiga spana nzito kwa hoja yake hiyo.
Soma Pia:

- Ushauri wa Gerald Hando kuhusu tiktok ni mwiba kwa uhuru
- Kuelekea 2025 - UVCCM waitaka Serikali kuifungia X (zamani Tittwer)