Wewe Acha janja janja hata huitwe mohamed na akuna jina unique duniani mzee ana miaka 60 tufanye kaenda huko na miaka 30 so itakuwa KWA makadirio kaenda 90s so miaka 30 iliyopta idara inakosaje kumbukumbu za muda kama huo??
Seems like hujui watu walikuwa wanaenda vipi mbele miaka ya nyuma....
FYI, moja ya changamoto wanazopata balozi zetu za nje ni kutokuwa na idadi sahihi ya Watanzania waliopo huko!!!
Sasa tatizo linakuja inapotokea mtu amefariki au kutupwa jela!! Mamlaka za huko zinakuletea taarifa kwamba huyu ni mtu wenu lakini mkiangalia kwenye rekodi, hayupo kwa sababu aliingia kwa kujilipua, na kwahiyo ubalozi haumfahamu!!
Miaka hiyo hiyo, enzi wa-South waliokuwa Tanzania wanarudi kwao baada ya uhuru, kuna mwana mmoja kitaa, sijui alifanya fanya vipi, anajua mwenyewe!! Mshikaji akaondoka na wa-SA kama mtu wa South Afrika wakati ni Mbongo PURE kwa sababu, hata Bush, nyumba yao na ya kwetu zinatazamana!!
Kama ilivyo ada ya Wabongo, mwana kafika SA, akaanza kuuza powder. Moja ya trips zake akaenda Amsterdam akadakwa, na kula mvua!!
Now assume huyu angekutwa na umauti huko Uhalonzi au nchi yoyote... it's obvious, mamlaka za huko zingewasiliana na ubalozi wa South Africa!
Ubalozi wa South Africa ungehangaika kutafuta ndugu zake huko SA, na wasingewapata na labda katika tafuta tafuta hiyo wangegundua kwamba mwana ni Mbongo!!!
Hatimae taarifa zingefika ubalozi wa Tanzania ambao hakuna records zake, na kwahiyo wangelazimika kufanya kama walivyofanya hao wa Ufaransa!!
Na mfano mwingine, ni kama pale Wanyarwanda waliokuwa ukimbizini TZ walipopelekwa Canada!!
We unadhani hakuna Wabongo ambao walijichomeka mle?! Na kama wapo, unadhani ubalozi wa Tanzania nchini Canada watakuwa na taarifa zao wakati wameenda huko kama Wanyarwanda?