Mtanzania Ahady amepata timu ya Forza Footbal Club ambayo inazalisha wachezaji na kuwauza kwenye mataifa mbalimbali

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
224
Reaction score
236
Anaandika Mo Mlimwengu.

Wakati Christopher Columbus akizunguka ulimwengu mzima kwa ajili ya kutafuta makoloni ya kutawala na akiamini kwamba dunia ni duara. Hapa Tanzania kuna kijana mdogo kutokea Muleba ambaye kaamua kufuata nyayo za Columbus lakini kwa mission tofauti. Mission yake ni kuona anafuta kauli ya Rais Mwinyi kwamba timu ya mpira ya Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu.

Safari yake ilianzia kwenye kituo cha mpira cha vijana under 10 kikiwa chini ya Hosea na baadae akaanza kucheza Muleba Stars chini ya Kocha Khalid akiwa bado mdogo sana.
Alivyoanza masomo ya sekondari akahamia Ushirombo ambako nako aliendelea kukipiga kwenye timu tofauti tofauti kwa madaraja. Kwenye mashindano ya Umiseta alichaguliwa kwenda kuwakilisha kitaifa na hapo ndio alipata nafasi ya kufanya trial kwenye kituo cha Alliance sports Academy Mwanza na akafaulu na kuanza kucheza pale.

Mtafutaji siku zote huwa hachoki kijana Ahady baadae alijiunga timu ya Simba ya vijana chini ya Kocha Niko Kiondo. Baadae akaenda kufanya trial timu ya ligi kuu ya Polisi Tanzania kwenye senior timu hakupata nafasi licha ya kufaulu trial. Wakati mwingine huwa nasema huwa ana ujasiri kama wa siafu athubutuye kuvuka mto kwa kupanda siafu wenzie mgongoni. Alivyorudi hakuwa kwenye timu yeyote akawa anafanya mazoezi binafsi mtaani na timu mbalimbali.

Wakati dunia inaendelea kulizunguka jua na Ahady naye anapambana kupata timu ya kucheza mpira. Alipata nafasi ya kucheza timu ya Buhaya Football Club ambayo makazi yake ni Kagera. Kipindi ambacho yupo Buhaya alipata nafasi ya kucheza mechi ya kirafiki kati ya Buhaya na Kagera Sugar. Ahady alitembeza boli kama asemavyo Mgunda boli litembee. Mpira ni mchezo wa wazi meneja wa U.R.A timu ya Uganda aliona dhahabu mchangani. Hakuwa tayari kuacha kipaji chake. Hivyo aliondoka naye kwenda naye nchini Uganda kucheza timu ya vijana.

Wakati Zuchu anamtafuta honey wake huku Ahady anatafuta kwa hali na mali kutimiza ndoto yake. Passport zikagongwa na visa akapata safari ya kuelekea ughaibuni ikawadia. Alienda Dubai na kuanza kufanya trial kwenye timu mbalimbali. Kuna timu ikampata lakini kutokana na sheria za Dubai hawezi kucheza kwenye timu za ligi kuu mpaka awe amefikisha miaka 18. Hiyo timu ikampatia nafasi kwenye Academy kubwa na ya gharama hapo Dubai kwa ajili ya kulea vipaji kwa timu za vijana. Ninavyoandika sasa Ahady amepata timu ya Forza Footbal Club ambayo inazalisha wachezaji na kuwauza kwenye mataifa mbalimbali.

Mlimwengu mimi natumia nafasi hii kukupongeza na kukutia moyo. Ndio kwanza picha limeanza ninaamini ipo siku narudia tena ipo siku na siku hiyo yaja ya kuvaa jezi la taifa letu Tanzania na kupigania taifa lako uwanjani.

All the best Ahady Mohamed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…