Mtanzania ajivunia kucheza dhidi ya Andre Ayew

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Kiungo wa SK Sturm Graz, Mtanzania Michael Lema amesema anajivunia kupata nafasi ya kucheza dhidi ya kiungo wa Ghana na West Ham, Andre Ayew.

Katika mchezo huo wa maandalizi ya mwanzo wa msimu uliofanyika kwenye Uwanja wa Thermenstadio ulishudia timu hizo zikitoka suluhu.

Lema alisema Ayew ni moja ya mastaa wa Afrika wanaomvutia na mara baada ya mchezo huo aliona ni bora kuzungumza na nyota wa Ghana.

“Nilimwendea na kujitambulisha kwake alinichangamkia na nilimuomba aniambie jambo ambalo linaweza nisaidia kwenye soka langu, alitabasamu na kuniambia kuwa hakuna linaloshindikana penye nia," alisema kinda huyo.

Katika mechi hiyo Lema alicheza katika dakika zote tisini na kupambana na mabeki Pablo Zabaleta na Sam Byram wa West Ham.

Source : Mtanzania ajivunia kucheza Ayew

Player Profile : Michael John Lema - Spielerprofil 17/18
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…