Mtanzania aliyeuawa vitani Urusi; kifo cha kishujaa?

Mtanzania aliyeuawa vitani Urusi; kifo cha kishujaa?

Anna Nkya

Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
69
Reaction score
341
Nemes Tarimo alienda Urusi kusoma mnamo mwaka 2020. Akiwa huko Urusi, mwezi Machi 2022 alikamatwa kwa uhalifu akahukumiwa miaka 7 jela.

Warusi wakatoa ofa kwa wafungwa kwamba ukienda vitani, baada ya vita utapewa fedha nyingi na utapata uhuru. Nemes Tarimo akajiunga na kundi la Wagner Group akaenda vitani na kufia huko.

Leo (Januari 24,2023), mwili wake unasafirishwa kutoka Urusi kuja Tanzania.

Najiuliza, hivi ni sahihi kusema amekuwa kishujaa? (kwa maana kwamba ameenda ugenini, akapmbana na bahati mbaya akaangukia jela, kisha akasema aende vitani tena kupambana hadi umauti ulipomfika...)

maxresdefault.jpg
 
Shujaa ni Muhammad Ali alikataa kwenda vitani bila sababu za msingi
Ukiangalia vita kwa undani ni: "vijana ambao hawachukiani lakini wanauana kwasababu ya wazee wanaochukiana" (sijui nilisomaga wapi hii?)

Ona sasa Nemes kadedi ila Putin yupo zake anaendelea kula bata huku familia kaificha sehemu huko..
 
Back
Top Bottom