Mtanzania aliyewahi kuchezea Simba ang'ara Ujerumani

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Mtanzania Emily Mgeta ameiwezesha timu yake ya VfB Eppingen kuibuka na ushindi wa kwanza akiwa anaichezea kwa mara ya kwanza katika mashindano.

Mgeta ambaye ni beki wa kushoto wa zamani wa Simba ameonyesha kiwango cha juu wakati VfB Eppingen ikiitwanga TSG Weinheim kwa mabao 2-1 katika mechi ya Kombe la Ujerumani.

Mechi hiyo ni kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Ujerumani maarufu kama Germany Polka.
Mgeta alicheza kwa dakika zote 90 huku akiongoza kwa kupiga krosi nyingi langoni mwa TSG ambao mwanzoni walionekana kama watashinda mechi hiyo kabla ya mambo hayajawageukia.
Kawaida, timu za madaraja mbalimbali hucheza michuano ya awali kupata nafasi hiyo.

Mgeta ambaye amekulia kisoka mkoani Mwanza, amejiunga na timu hiyo ya VfB Eppingen msimu huu

Chanzo:Saleh Jembe
 
kacheza simba mwaka gani mbona jina geni hili
 
akomae.. safar bdo ndef.

mx_nature
 
Wabongo bwana eti nilidhani bayern Munich angekuwa hata Academy ya bayern angeshakuwa superstar Wa bongo.ila si haba hata timu za madaraja ya chini wanaviwango kupita timu zetu za primier league


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…