Inauma sana jamani!unaweza ukasema why GOD!Lakini ndo hivyo tena tumebaki na majonzi
tu!Muimbaji aliyeimba "kifo hakina huruma" hakukosea!Yaani kifo kilishindwa kumuhurumia huyu kijana mzuri aliekuwa hajafanya kosa barabarani!waliofanya kosa wakapona!
MUNGU amuweke mahali pema peponi!Ameni
Kwa kumbukumbu yangu huyu ni mwana-JF wa tatu anatutoka baada ya Makene na yule dada wa Dar. Mungu awatulize wote waliofikwa na msiba huu, awajaalie moyo wa ustahimilivu na subira. Na wote waliofariki dunia, Mungu ndiye ajuaye imani na ibada zao, maana Yeye ajua yote, na mapenzi yake hutimia. Amina.
Wafiwa na wana JF pia poleni.
Kwa wote mloshiriki kwa hali yeyote ile well done na muendelee na mioyo hiyo- Ninyi ndo mnayoifanya dunia iwe mahali pazuri pa kuishi.
Marehemu Ndalima anatarajiwa kusafirishwa leo (Jumanne) kupelekwa nyumbani kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi. Hili limewezekana kwa michango ya Watanzania kutoka sehemu mbalimbali duniani ambayo iliwezesha kufikia lengo letu la kupata dola 16,000 nda ndani ya siku tano tangu tuanze tulifikia lengo hilo jana. Tunaendelea kuwashukuru kwa michango yenu na taarifa rasmi itatolewa baadaye.
Polen sana wote
tutaomba wahusika wa hapa tanzania tujulishane msiba uko sehemu gani???
Na matarajio ya kufika dar es salaam lini na saa ngapi,mungu awatie nguvu
wote!!!
Shukran Mkuu Ab-Titchaz na jamaa wote wa Detroit kwa habari na shughuli zote zilizomuhusu mwenzetu Ndalima.Mwili wa marehemu ulifika salama nyumbani na alizikwa Jumamosi ya tarehe 25/10/08 huko kwenye makaburi ya Chang'ombe.Mazishi yalihudhuriwa na ndugu,wanafamilia na marafiki wengi.Tuuendeleze moyo huu wa kujaliana na kusaidiana ni mwenyezi Mungu tu mwenye uwezo wa malipo kwa wema mnaoutenda!! Amen...