Mtanzania atunukiwa udaktari wa heshima na Chuo cha Oxford Club Awards

Mtanzania atunukiwa udaktari wa heshima na Chuo cha Oxford Club Awards

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mtanzania Diana Laizer ametunukiwa udaktari wa heshima na Chuo cha Oxford Club Awards huko London nchini Uingereza kutokana na mchango wake kwenye jamii kupitia tuzo za Chaguo la Mtumiaji Afrika.

Diana ambaye ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa tuzo hizo maarufu Consumer Choice Awards, ametunukiwa udaktari wa heshima katika biashara na ujasiriamali kwa kuonesha jamii kuwa kijana anaweza kujitengenezea ajira na kuajiri wengine.

Akizungumza na Mwananchi, leo Alhamisi, Desemba 5, 2024 akiwa London amesema sababu nyingine ni pamoja na mchango wake kwa miaka sita kwenye tuzo hizo ambazo zimeongeza ushindani wa utoaji huduma bora kwa watumiaji hapa nchini na nje ya nchi.

Tuzo hizo zimelenga mtumiaji na mtoa huduma ili kuongeza thamani ya ubora wa bidhaa na huduma kati yao amesema: “Mchango wa ushiriki kwa miaka zaidi ya sita ndiyo chanzo kikubwa cha kupata udaktari wa heshima.”

Aidha kitendo cha kuthubutu kujiajiri, kutengeneza ajira kwa wengine na taasisi hiyo kuajiri vijana, kutambua mchango wa tuzo hizo kwa wafanyabiashara na uwekezaji hapa nchini ni miongoni mwa mambo yaliyombeba.

Screenshot 2024-12-05 213254.png
 
Hongera zake sana aendelee kuliwakilisha vema taifa, ebu tupia kapicha japo huku Sumbawanga tumfahamu
 
Back
Top Bottom