MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mtanzania avunja rekodi kwenye mbio za Valencia Marathon
Leo tarehe 4/12/2022, mtanzania Gabriel Geay (26) aweka rekodi mpya ya taifa kwa mbio za km 42 (Marathon) huko Valencia, Spain. Geay kamaliza mbio hizo akiwa wa pili kwa muda wa masaa 2:03:00 ambayo ni muda wake binafsi bora zaidi pia ikiwa ni rekodi mpya ya taifa.
Ikumbukwe rekodi iliyovunjwa ya muda wa masaa 2:04:55 iliwekwa na Gabriel Geay pia. Kavunja rekodi yake mwenyewe. Katika umri wake wa miaka 26 tayari Gabriel anashikilia rekodi za taifa kwa mbio za 15km, 20km, 21km (Half Marathon), 25km na 30km. Tukimtoa Mzee Filbert Bayi, huyu kijana ni mtanzania mwingine anayeshikilia rekodi nyingi kwenye riadha kitaifa.
Valencia Marathon haikuwa rahisi kwasababu mshindi Kelvin Kiptum kutoka Kenya naye kaweka rekodi mpya ya Valencia Marathon (course record) kwa muda wa masaa 2:01:53 ambapo kwa hapa duniani aliyemzidi ni mtu mmoja tu. Ambaye ni Eliud Kipchoge mwenye rekodi ya dunia ya masaa 2:01:39. Kwahiyo hata kijana wetu yuko jirani kabisa na rekodi ya dunia yeye akiwa namba 3 kidunia kwa mujibu wa shirikisho la riadha la dunia. Akikaza anaivunja. Link hii hapa orodha ya wakali wa Marathon duniani World Athletics | Marathon - men - senior - outdoor - 2022
Pamoja na medali ya fedha, kijana wetu atatia kibindoni zawadi ya Euro 45000 yaani kama Tsh 110,000,000/= ikiwa ni zawadi kwake. Wazazi msapoti vipaji hya watoto wenu. Kwenye vipaji kuna hela nyingi sana. Geay kapiga hiyo 110m leo lakini kumbukeni kijana ana mkataba na Adidas pia anashiriki mbio kubwa sehemu mbalimbali duniani. Isitoshe kwa kuwa kashakuwa supastaa atakuwa analipwa Appearance Fee kila akialikwa kushiriki. Yaani ana bonus nyingi tu. Inawezekana kwa kushinda hivyo leo akatengeneza hata 300m kwa leo tu.
Hapo chini ni matokeo ya mbio za Valencia Marathon.
1.Kelvin Kiptum 2:01:53 🇰🇪 CR
2.Gabriel Geay 2:03:00 🇹🇿 PB/NR
3.Alexander Mutiso 2:03:29 🇰🇪
4.Tamirat Tola 2:03:40 🇪🇹
5.Ozbilen Kigen 2:04:36 🇹🇷
6.Deso Chalu 2:04:56 🇪🇹
7.Mengesha Milkesa 2:05:29 🇪🇹
8.Ronald Korir 2:05:37 🇰🇪
9. Philemon Kiplimo 2:05:54 🇰🇪
10.Goitom Kifle 2:06:29 🇪🇷
Nimefurahishwa sana na ushindi huu. Namshukuru na kumpongeza mwenyekiti wa CCM Mama Samia kwa ushindi huu. Kwa uhamasishaji wake kijana kaenda kushinda. Nampongeza pia Gabriel Geay kwa ushindi huu. Namsihi aendelee kuishi maisha yake ya kawaida na kujiepusha na mambo ya kipuuzi kama walivyo vijana wengi maarufu. Hivi cocastic, mzabzab huyu kijana angekuwa mshenzi angetafuna bongo movie wangapi kwa mpunga anaotengeneza?