Mtanzania Geay avunja rekodi ya Daegu Marathon, South Korea

Mtanzania Geay avunja rekodi ya Daegu Marathon, South Korea

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Leo tarehe 23/02/2025 huko nchini Korea Kusini bendera ya taifa imepeperushwa vyema na kijana Mtanzania Gabriel Geay kwa kuvunja rekodi ya mbio za Daegu Marathon (course record) kwa kutumia muda wa masaa 2:05:20 na kuibuka wa kwanza. Ikumbukwe Geay ndo anashikilia rekodi ya taifa ya marathon kwa muda wa masaa 2:03:00 kupitia Valencia Marathon ya mwaka 2022. Hapo chini nimekuwekea matokeo ya nane bora.

Daegu Marathon 2025 results (top eight):
Men's elite race

Gabriel Geay (TAN) 2:05:20
Addisu Gobena (ETH) 2:05:22
Dejene Megersa (ETH) 2:05:59
Ogbe Kibrom Ruesom (ERI) 2:06:04
Othmane El Goumri (MAR) 2:06:07
Gilbert Kibet (KEN) 2:06:39
Stephen Kiprop (KEN) 2:07:16
Sezgin Atac (TUR) 2:07:26

Geay ni mfano wa kuigwa miongoni mwa wanamichezo wa taifa hili. Huyu ni miongoni mwa wanamichezo wachache sana wasomi hapa nchini. Nje ya riadha nafurahishwa mno na jinsi anavyorudisha kwa jamii kupitia riadha. Siku za hivi karibuni ameanzisha charity organisation inayojulikana kama Geay Foundation kwa nia ya kusaidia mambo mbalimbali hasa kuinua vipaji vya watoto wenye vipaji vya michezo. Yuko tofauti na wanamichezo wengine wanaorudisha kwa jamii kwa kujenga misikiti na makanisa badala ya kusaidia fani zilizowainua wao.

Ninatarajia hakutakuwa na mizengwe kwenye hii foundation yake ili taifa linufaike. Miaka iliyopita kulikuwa na shirika la Shoe 4 Africa from America lililokuwa linasapoti mambo ya riadha ila walishindwana na wabongo wakaamua kuweka nguvu Kenya ambako hadi leo wanafanya makubwa. Unaweza ku-google kuhusu Shoe 4 Africa.
 

Attachments

  • FB_IMG_1740312611493.jpg
    FB_IMG_1740312611493.jpg
    76.4 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740312614488.jpg
    FB_IMG_1740312614488.jpg
    60.6 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740312715267.jpg
    FB_IMG_1740312715267.jpg
    55 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740312717990.jpg
    FB_IMG_1740312717990.jpg
    48.1 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740312722289.jpg
    FB_IMG_1740312722289.jpg
    58.6 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740312743008.jpg
    FB_IMG_1740312743008.jpg
    42 KB · Views: 1
Hizo mbio zingeitwa Samia Marathon ingekuwa mwake. BTW Guay amshukuru mama kwa kuleta mashindano
 
Back
Top Bottom