Mtanzania hatarini kuuwawa huko Uingereza

Sheria za Uingereza na vyombo vya dola vilishughulikie ipasavyo.
Ni ukiukaji wa haki za binadamu kuingilia Uhuru wake wa kuishi kwa kumpa vitisho ashiria kuhatarisha maisha ya mtu sio swala dogo .Mungu amlinde Hugo Mtanzania mwenzetu.
 
Nilivyomsikiliza ni kama hana akili timamu ni haki yake kunyanganywa watoto.
 
Sio Chahali huyo? Mwenyewe hupenda kujiita Jasusi
 
Any dispute inayohatarisha maisha ya raia ya nchi fulani lazima balozi husika ilishughulikie .
Lakini si ana uraia wa uingereza? Kisheria yeye siyo raia wa Tanzania kwasababu hatuna dual nationalities. Kwa iyo polisi uingereza ni jukumu Lao.
 
Raia wa Uingereza anawahusu nini? Si wenyewe wamegoma kuwatambua watu waliochukua. Uraia wa nchi nyingine? hicho kiherehere kinatoka wapi?
 
Raia wa Uingereza kutishiwa Maisha nchini kwake sisi Tanzania inatuuma sana mpaka Balozi wetu ashughulike kiasi hiki?

Huyu Mama tuna maslahi gani naye
kama Taifa?
 
Hizo ni domestic disputes. Kwanini balozi apoteze muda na hela kusuluhisha? Si kuna polisi na huyo ni raia wa uingereza? Sisi hatuna dual citizenship.

Black Sniper Mudawote RRONDO
Ukiteuliwa kuwa Balozi nchi za kuwakilisha mchi za Kiafrika hasa Tanzania, ni sawa na Kamanda wa Polisi wa mkoa (RPC) kurudishwa Makao Makuu kusoma magazeti. Mabalozi wa hizi nchi zetu kule huwa hawana kazi at all.
Unaweza kukuta Balozi mzima na maafisa wanawahi na kushinda ofisini wakiangalia clips za babu wa TikTok, mara mwingine awashe muziki kwa sauti wanaanza kuyamwaga mauno.
Kazi ina sound vizuri sana, ina tone nzuri lakini ukifika ubalozini ni vituko tu.
Ndiyo maana Kairuki kaamua ku force kazi za kufanya ili aende mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…