DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Waacheni wazungu waendelee, linapokuja suala la mtu wa kwao watafanya juu chini apate msaada. Nafanya kazi ubalozi wa nchi moja ya Nordic, yaani wakisikia tu hata kuna ajali imetokea na kuna mzungu humo ninlazima wafuatlilie kujua kama kuna mwananchi wao humo.

na kama yupo, fasta anapatiwa msaada . Kiufupi, wenzetu wanajali sana.
 
Ni kweli kabisa mkuu, lakini lazima ana watu wake nyumbani
Hili suala ni jukumu la Balozi ila kama wao ndio wana majibu ya kijinga hivyo basi hawajui wajibu wao
Ndio hao wanapewa kazi ya Ubalozi halafu wanachukua ndugu zao wakajaze nafasi hata ya usafi
Kelele zimepigwa sana na mimi nikaona bora achangiwe na kama itakuwa vizuri basi hata apelekwe hospitali kwa michango, na serikali Ibanwe kwa kelele
Na huyo Dr Dorothy aione hii na amwage chozi Bungeni kama last week
 
Kuna dogo mmoja, aliunganishwa kwenye exchange program ya vyuo, ana uncle wake pale SUA (Prof) alimuunganisha ingawa yeye alikuwa tayari graduate tena wa chuo kingine kwenda US kusoma.

Alipofika US ili project haikuwa kwenda kusoma ilikuwa ni kazi. Huyu dogo alikuwa anamsumbua sana uncle wake kuhusiana na siala la ajira au mchongo wa kusoma.

Fast forward, kafika US kakuta ile ni kazi, ya kusafisha mabanda ya farasi.

The first few weeks, ali-undergo depression, kulia karibu kila siku (mtoto wa kike), ila baada ya miezi kadhaa kazoea.

Inshort dogo ananunua plot tu huko kwao Geita hivi sasa kama kichaa, yeye anapambana na kununua plot, ufugaji anafanya kazi bega kwa bega na mama yake.

TZ wengi wanajua anasoma lakini kwenye ground anapiga usafi tu. Na sasa kapata mchongo wa namna hiyo hiyo Canada, wanamlipa vizuri zaidi.

Kakubaliana na hali, na pesa anayopata ni nzuri.

Haya ma ukichaa huwa mengi yanaletwa na depressions, huna pa kushika, life style uliyokutana nayo tofauti, utu tofauti, hence unashindwa ku-hold mambo, unadata.
 
Ni wazo zuri, lakini hizi nchi za wenzetu, huwezi kumshutisha mtu arudi nyumbani bila hiari yake. Sasa, ukiunganisha na maradhi ya akili ndio kabisa. Cha kwanza nadhani ni tiba halafu hayo mengine ndio yatafuata. Ni suala Tata sana lisilokuwa na
Jamii forum inatakiwa iwe strict kwa hili, huwezi kuanika personal information kwenye Public forum, ni kosa hili.
Nivyema sana Kama hujui jambo ukawa kimya huyu dada kuna wakati anavua nguo mbele za watu Mimi mwenyewe nimempelekea nguo na chakula huko porini ili kumsitiri mbona information zangu nimetoa nichukulie hatua wewe basi narudia Tena kwa watanzania wenye akili timamu huyu dada anahitaji msaada sikukurupuka
 
Ingekua hivyo basi kungekua hakuna deportation watu wanarudishwa makwao na pingu je nihiari yao? Nchi gani hizo au za ahera 😂😂
 
Kwa Hiyo Balozi Wetu Kapata Taarifa Ila Anaendelea Kula Kiyoyozi. Mtanzania Mwenzetu Hamthamini. Au Huo Ubalozi Ajishughulishi Na Maswala Hayo?
 
Jamii forum inatakiwa iwe strict kwa hili, huwezi kuanika personal information kwenye Public forum, ni kosa hili.
Sasa hebu angalia, huyo dada aliyetajwa kwa hilo jina hata mimi nimeenda kumgugo na kumkuta kwenye mitando ya jamii wakati huo amesoma, na ni kweli alisomea sheria UDSM,
Huu ni udhalilishaji, nashangaa Maxence Melo yuko kwenye tume ya kulinda taarifa binafsi za mtanzania, lakini wafanyakazi wake wanamuangusha
 
kausha s tumempeleka huko km undercover ndio maana ubalozi wamevunga
 
Usikute ndugu zake huku huku Tanzania ndiyo wamemfanyia haya kwa wivu........kingine, balozi za Tanzania hazina watu wanaojitambua, wengi wao hawajuwi wanafanya nini haswa waishio huko Marekani ni kama wamepelekwa tu kushangaa miji.
 
hivi hatuna ubalozi marekani, wanafanya nini huko au wanakula tu kodi zetu?
Balozi tunazo 2, ila wafanyakazi wa balozi zetu ni mambumbumbu kinoma na waliojawa na wivu kwa sababu hawalipwi mshahara mzuri, unakuta diplomat mzima analipwa mshahara wa mtu asiyesoma au kuwa na college degree. Naishauri serikali wawe wanatoa tours tu za miaka 2 miwili maana diplomats wetu wako very useless na ndiyo maana Magufuli alikuwa anawapiga vita na kuwapa challenges.
 
huwa najiuliza, hivi ikitokea Mmarekani mmoja tu, amekuja Tanzania akapata shida yeyote, ndani ya siku hiyo hiyo utakuta ubalozi wa Marekeni umeshachukua hatua. sasa balozi zetu nje huwa zina faida gani? au wanatafuta tu wawekezaji ila raia wao sio wa muhimu sana. sawa na baba anatafuta chakula kwa ajili ya watoto ila hawajali watoto wenyewe, chakula unatafuta kwa ajili ya nini sasa kama sio kwa ajili ya Watoto/watanzania raia? hao wawekezaji wana faida gani kama raia wako unaotafuta kuwaboreshea maisha kwa kuleta wawekezaji hauwajali?
 
Unavyoona jinsi bunge letu lilivyo useless kwa kuwa na wabunge vilaza ndivyo zilivyo balozi zetu nje......yaani madiplomat wetu wako very incompetent, wakirudi Tanzania kiingereza kingi lakini hawajuwi wajibu wao.
 
Mbona barua imeandikwa na Masilingi na tarehe ni 2018 huko??? Saivi yuko bi Kanza, ni nini sijaelewa hapo?
Ndiyo. Hii habari ilitoka miaka ya nyuma. Sijui huyu mwanzisha thread ameiokota wapi akai-post tena au labda huyo dada bado hajapata msaada hivyo amekumbushia.
 
Mbona unakuwa kama huna akili? Hujaahi kuona vichaa wengi tu wanaomba fedha na wanajua matumizi yake?
 
Kama una exposure namna hiyo na unajua kuwa balozi zinatakiwa zijue watu wao, unashindwaje kuona umuhimu wa huyu member anayetafuta ndugu wa huyo msichana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…