Mtanzania ijue haki yako: Je, Polisi anayo haki ya kupekua simu yako bila search warrant?

Mtanzania ijue haki yako: Je, Polisi anayo haki ya kupekua simu yako bila search warrant?

politiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Posts
2,376
Reaction score
1,508
kumeibuka tabia ya polisi hivi karibuni kuwakamata watu kwa makosa na kuwapekua na wakiwakuta na simu basi uanza kupekuwa simu zao kujifanya kuwa wanatafuta ushahidi fulani.

Je, kwa polisi kufanya hivyo hawavunji sheria mama ya nchi kwa maana ya katiba ibara ya 16 kinachohusu privacy hasa ukizingatia kuwa simu kama i-phone ina personal information kibao kama sehemu ulizotembelea kwa kuwa ina GPS, watu
unaowasiliana nao, message za jamaa na marafiki.

Ibara ya katiba inasema:

Haki ya faragha na usalama wa mtu
Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.
Kwa mujibu wa ibara ya hapo juu cellphone inaweza ku fit kwy maelezo ya mawasiliano binafsi ingawaje sheria imekuwa ikitumika sana kuashiria zaidi kwy makazi ya mtu kuwa inahitajika search warrant lakini cellphone ina fit kwenye maelezo ya "mawasiliano binafsi" polisi anahitajika kuwa na search warrant kabla ya kupekuwa simu na kusoma kilichomo naomba mwenye hoja tofauti tuelemishane.

Naomba kuwasilisha.
 
Simu mbona kitu kidogo, siku hizi wameruhusiwa hAdi kututandika risasi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Simu mbona kitu kidogo, siku hizi wameruhusiwa hAdi kututandika risasi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

huko ni kuvunja sheria za nchi na ndio maana mhusika kafikishwa mbele ya pilato. i feel so proud to be one of many who signed that petition just to show so called "leaders" that we the people are watching them.
 
Wanakuvua nguo, wanaweka chupa ukalie ili useme Dr. Slaa, Mbowe, Mnyika, Lissu ndo magaidi... Ccm ndo master mind wa haya yote
 
Mh in the first place walikukamata kwa kosa/tuhuma gani?
 
Mkuu Politiki, mbona uzi unelekea kwingine tofauti na hoja ya msingi? Au ndo imejijibu yenyewe na hakuna haja ya mchango zaidi?
 
Kisheria polis hatakiwi kuchukua kitu chako chochote sababu simu haiongei na wala haijafanya kosa wewe ndio umefanya makosa lakin polis wakibongo hawajui sheria wengi wao ni darasa la 7 kwahiyo kuwampole tu
 
Back
Top Bottom