Polisi mjini Dallas wameomba msaada wa kumpata mtuhumiwa wa mauaji ya mhamiaji kutoka Tanzania, Johnson Mdoe Mchaina ambaye alikuwa anafanya kazi usiku kusaidia familia yake iliyopo Tanzania anapotoka.
Hivi ya CCTV inamuonyesha mtuhumiwa akimpiga risasi Johnson na kuchukua maisha yake. Tukio hilo lilitokea saa 8:45 usiku tarehe 9 July 2020 ambapo muuaji alimkuta Mdoe yuko peke yake.
Wafanyakazi wenzie wamemuongelea Mdoe kama mtu mzuri sana na alikuwa na mtoto wa kike nchini Tanzania na alijitahidi sana kumhudumia.
Mtuhumiwa ambae alikfika kufanya tukio la uhalifu alimuamuru Mdoe kwenda kwenye Rejesta, akiwa nyuma ya kaunta huku mhalifu huyo akiwa na wasiwasi na kutoishikilia vizuri silaha yake.
Mdoe alimfungulia trei na mhalifu kuchukua pesa lakini alishindwa kumfungulia ya pili, alitumia sekunde kadhaa na alionekana kuwa na hofu wakati silaha ikiwa inamzunguka na ghafla akapigwa risasi.
Mdoe alijaribu kumshika mtuhumiwa, aligeuka na kumpiga risasi, alisema Lopez ambae ni afisa wa polisi. Imetangazwa malipo ya dola 15,000 kwa taarifa itayopelekea upatikanaji wake na afisa wa polisi ana imani kuna mtu anajua jina lake au jina la utani.
Afisa upelelezi kasema, baada ya kutii amri za awali za kumpa hela, marehemu alijaribu kumpora bastola jambazi. Ikapelekea kuuawa kwake. Labda hapo kuna somo la kujifunza.
7-11 nao nadhani wana kesi ya uzembe ya kujibu. Mtumishi alikuwa peke yake dukani. Hakupaswa.
Afisa upelelezi kasema, baada ya kutii amri za awali za kumpa hela, marehemu alijaribu kumpora bastola jambazi. Ikapelekea kuuawa kwake. Labda hapo kuna somo la kujifunza.
7-11 nao nadhani wana kesi ya uzembe ya kujibu. Mtumishi alikuwa peke yake dukani. Hakupaswa.
Polisi katika jiji la Dallas, Texas nchini Marekani imeahidi kutoa takribani dollar za kimarekani 15,000 sawa na shilingi za kitanzania takribani 35mil kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu aliyemuua kijana wa kitanzania Johnstone Mchaina Mdoe.
Mdoe aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu aliyefunika sura yake mnamo Mwezi wa July.9.2020 kwenye duka alilokuwa akifanyia kazi.
Pole kwa ndugu na wote wanaoguswa na msiba msiba huu.