Gladness Ndahani
New Member
- Jun 14, 2024
- 1
- 1
MTANZANIA MWENYE TANZANIA TUITAKAYO
Je, ni nani mwenye Tanzania tuitakayo?
Ndugu msomaji, natamani tuzungumzie kwa pamoja suala la Tanzania tuitakayo. Leo hii utakubaliana na mimi kuna idadi ya watu wanao tamani sana kuishi maisha yao nje ya Taifa hili la Tanzania. Una weza ukawa ni mmoja wao au la. Lakini ukweli ni kwamba Tanzania ina idadi ya watu wasio furahia kuwa ndani ya nchi hii kuna wengine wametunga misemo kama vile;” bongo bahati mbaya, ni heri uwe mbwa ulaya kuliko kuwa bosi Tanzania “n.k Natumaini misemo hii sio migeni katika masikio yako. Taifa lina undwa na watu wenye majuto juu ya taifa lao na wamekuwa wakilaumu kila jambo linalo endelea katika taifa hili.Hivyo nipende kusema kama mmoja wa wanafalsafa alivyo wahi kusema “WE ARE THE CHANGE WE NEED” yaani sisi Watanzania ndio mabadiliko tuyatakayo.
Maamuzi ya kuifikia Tanzania tuitakayo yapo mikononi mwa Watanzania maana wao ndio wamebeba maana halisi ya Tanzania tuitakayo na si mtu yeyote yule kutoka nje ya Tanzania. Barack Obama katika moja ya kauli zake ame wahi kusema “To change America, you must Understand America “Hivyo nami nina sema ; “ Kuibadilisha Tanzania , lazima uifahamu na kueilewa Tanzania .
Nini jamii ya Watanzania ifanye ili kuifikia Tanzania tuitakayo ndani ya miaka mitano mpaka ishirini na tano ijayokupitia nyanja ya ELIMU?
1: Kuwekeza katika elimu inayowawezesha wasomi kushiriki katika nyanja mbalimbali hapa nchini.
“Ukimhukumu samaki kupitia uwezo wake wa kupanda mti, ataishi maisha yake yote akiamini kuwa yeye ni kiumbe mjinga kuliko wote ulimwenguni”- Albert Einstein
Ni muda mrefu sasa nguvu kubwa imekezwa katika elimu ya darasani pekee katika taifa letu la Tanzania. Hii kupelekea watu wengi kuamini uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko upo katika mfumo wa elimu ya darasani.
Jamii inahitaji elimu ya kuwawezesha wananchi wote katika Nyanja zote, hii itapelekea kila mmoja kukiamini kitu anachoweza kukifanya na hata kumsaidia mtu huyu kufanikiwa katika eneo hilo.
Ni taasisi chache za elimu zinazowawezesha watu hasa vijana kukuwa zaidi katika maeneo yao ya ujuzi, vipaji, karama mbalimbali.
Kupitia mitaala ya kielimu ndani ya taasisi mbalimbali za kielimu, ni mapendekezo yangu kuwa watu wapewe elimu zaidi ya zile wanazozipata madarasani kwa maana maisha halisi yapo nje ya darasani. Ndani ya miaka mitano mpaka ishirini na tano, tunaweza wekeza katika kuwawezesha wananchi kujifunza na kuwa bora darasani pamoja na maeneo mbalimbali ya ujuzi na uwezo. Hii itamsaidia mtu kuitumia elimu yake ya darasani ipaswavyo katika kuleta mabadiliko katika jamii. Yaani kuondoa mipaka ya mitaala ya kielimu.
Na ni kweli watu hawa hawana akili na uwezo katika nyanja nyingine tofauti tofauti? Pia, ni jitihada gani jamii ina fanya kuwawezesha watu wanao feli mitihani yao ya Taifa?.
Kumwamini kila mmoja kutokana na uwezo alio nao.
2: Kuweka mipango ya kuwawezesha watu wanaoshindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao ya kuhitimu yaani mitihani ya Taifa.
Leo hii utakubaliana na mimi kuwa idadi ya wanaoanza elimu ya awali ni kubwa sana kuliko idadi ya wanao hitimu vyuo na vyuo vikuu.
Je, wale wote walioamini katika elimu hata wakaanza lakini hawajafikiwa kufika mbali zaidi wanapewa kipaumbele gani katika kuleta mabadiliko na mchango katika jamii?. Ninatambua uwepo wa jitihada mbalimbali zinazofanyika kuwasaidia lakini ukweli ni kwamba bado nguvu kubwa inahitajika kwa maana wengi huishia kujaribu kujitafutia kipato kwa kufanya shughuli mbalimbali mtaani na kwasababu jamii ina amini yeyote aliye shindwa kufaulu ni mjinga , hivyo hata kazi wanazozifanya zinakuwa za viwango vidogo kwa maana hata jamii imetengeneza matabaka ya wasomi.
Ni muda sasa hata Mtanzania aliyeshindwa kufaulu na kujiendeleza kielimu apewe thamani katika jamii hasa pale anapoamua kujishughulisha na shughuli mbalimbali katika jamii kwa kupewa elimu inayotambulika kwa watu wote kuwa ni elimu ya kuwaendeleza watu wanaoshindwa kufaulu katika nyanja kama vile vipaji, uwezo na ujuzi na elimu hii ipewe thamani kama ilivyo elimu ya Sekondari pamoja na vyuo vikuu. Natambua uwepo wa taasisi za VETA hivyo nchi ina paswa kuwekeza zaidi katika taasisi mbalimbali zaidi na zikafikika kwa watu wote mjini na vijijini.
3: Ubora na viwango vya elimu kwa Watanzania wote.
Elimu bora ina gharamiwa, na ukiangalia shule nzuri za watu binafsi zinatoa elimu bora na kwa bahati nzuri au mbaya elimu hiyo hugharamiwa.
Uhalisia ni kwamba idadi lkubwa ya wanachi bado inapitia hali ya umasikini na maisha duni. Leo hii kuna mtu ana soma darasa la saba kwa ada ya milioni moja kwa mwaka, mwingine anasoma kwa milioni nne kwa mwaka na kuna mwingine ana soma bure kwa kuchangia ada ndogondogo kama hela ya mlinzi na bado familia ina pata shida kulipia vitu hivyo.
Idadi kubwa ya ndoto za watu wengi zimezikwa katika umasikini wa muda mrefu na imekuwa ni kilio cha wengi kutamani angalau wangepata nafasi ya kusoma vizuri ili kukomboa familia zao. Nguvu kubwa imewekezwa kwa watu wenye uwezo zaidi na kulisahau kundi kubwa la watu wenye maisha duni hali hii imekuwa hata katika upatikanaji wa kazi na fursa mbali mbali yaani nani ana mjua nani au ni mtoto wa nani bila hivyo kuna kazi ni ngumu kuzipata.
Si kwamba mtoto wa masikini ni mjinga, si kwamba hana uwezo ila ana kosa nafasi ya kuaminiwa katika kufanya makubwa zaidi. Atafanikiwaje ikiwa kuna tabaka kubwa la kuwatenganisha na wale wenye uwezo?
Ni maombi yangu nchi yetu ikaue matabaka haya ya umasikini na utajiri na tukaishi kwa kuthamini uwezo uliopo ndani ya watu tofauti tofauti bila kujali hali zao.
HITIMISHO
Kila mmoja ana tamani kufikia tamati ya hadithi ambayo maisha yake yote yatabadilika na kuwa bora zaidi ya yalivyo sasa THE STORIES OF CHANGE . Tuna tamani hadithi zetu za kuibadilisha Tanzania yetu zikawe ni hadithoi zenye uhalisia na mvuto kwa watu wengi ulimwenguni, hivyo tushirikiane kwa pamoja kuifikia Tanzania tuitakayo.
(Maneno 948 )

Upvote
2