Mtanzania UK amhifadhi Eboue nyumbani kwake kwa miezi mitatu

Mtanzania UK amhifadhi Eboue nyumbani kwake kwa miezi mitatu

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
‘NILIMWOKOA EBOUE SAA NANE USIKU’

Mtanzania , Yasmin Razak, ameeleza namna alivyokutana na nyota wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Emmanuel Eboue, kabla ya kumpa hifadhi nyumbani kwake.

Eboue alikutana na majanga hayo baada ya mahakama moja nchini Uingereza kutoa uamuzi wa kuvunja ndoa yake na aliyekuwa mkewe.

Mbali ya kuvunja ndoa hiyo, mahakama hiyo ilimtaka mchezaji huyo kuondoka katika jumba alilokuwa akiishi na familia yake pamoja na kunyang’anywa mali zake nyingine ili zikabidhiwe kwa mtalaka wake.

Akifafanua kwa kina sakata hilo jijini Dar es Salaam ambako yupo kwa shughuli binafsi, Yasmin, alisema kitendo kilichomtokea mchezaji huyo kinapaswa kuwa darasa kwa wanasoka wengine wa Afrika.

“Kimsingi mimi nafahamiana na wachezaji wengi nyota kule Uingereza hasa wa Afrika si Eboue tu, mimi ni kama dada yao na nimekuwa nikiwasaidia kwa mambo mengi ukiwemo ushauri.

“Kimsingi nilimhifadhi Eboue kwangu baada ya kutimuliwa katika nyumba yake kwa amri ya polisi, nakumbuka ilikuwa Januari mwaka jana aliponipigia simu saa nane usiku,” alisema Yasmin.

“Aliniambia sina pa kwenda, niliwasha gari nikamfuata, nikamchukua nikamleta nyumbani kwangu nikaishi naye kwa miezi mitatu, baada ya hapo alikuwa anaondoka na kurudi, wakati huo alikuwa anaenda kwa marafiki zake Waafrika wengine wanaoishi miji mingine.”

Yasmin anasema baada ya sakata hilo, alimtafutia mwanasheria ambaye alimsaidia kurudishiwa mojawapo ya nyumba zake na wakati huo walikata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kumpora mali.

“Ukiangalia matatizo yote haya yametokana na ukosefu wa elimu, kwani wakati mahakama inaendesha kesi, hakuweka mwanasheria, pia alikuwa haudhurii, hii ilikuwa fursa tosha ya mkewe kuidanganya mahakama,” alisema Yasmin.

Aliwataka wachezaji wa Afrika hasa wanaocheza soka barani Ulaya kuhakikisha wanakuwa na wanasheria watakaowasimamia mambo yao ikiwemo mikataba ili kuepukana na kilichomkuta Eboue.

“Kuna mengi yapo nyuma ya wachezaji wa Afrika, wengi hawajasoma kutokana na kutoka familia za kimasikini, wakipewa pauni 50,000 kwa wiki wanachanganyikiwa, wanapaswa wawe na wanasheria.

“Binafsi huwa nawasiliana sana na Mbwana Samatta, huwa namwelekeza mambo mengi,” alisema Yasmin ambaye ameweka makazi jijini London.
 
Mmhh ufahamu wangu mara nyingi kwenye kesi kama hizi, hata hakimu hutaka pande zote ziwe na wakili. Kuna rafiki zangu wengi sana wameachana na wake zao, na upande wa mume ukiwa na lawyer basi na mke nae lazima atatafuta lawyer. Bei za lawyer wale wazuri kwa kesi kama hizi huwa £ 1,500 mpaka £3,000 na hawa wachezaji lazima wawe na agent na huyo agent na lawyer wa huyo mchezaji ndio washauri kwa mambo mengi.
 
Kama eboue alikuwa haendi kuhudhuria kesi mahakamani. Kosa ni la kwake. Kama angekuwa anaenda asingepokonywa Mali zote.
 
Mmhh ufahamu wangu mara nyingi kwenye kesi kama hizi, hata hakimu hutaka pande zote ziwe na wakili. Kuna rafiki zangu wengi sana wameachana na wake zao, na upande wa mume ukiwa na lawyer basi na mke nae lazima atatafuta lawyer. Bei za lawyer wale wazuri kwa kesi kama hizi huwa £ 1,500 mpaka £3,000 na hawa wachezaji lazima wawe na agent na huyo agent na lawyer wa huyo mchezaji ndio washauri kwa mambo mengi.
Ushaambiwa alikuwa haudhurii mahakamani. Na hata mwwnasheria hajamuweka. Sasa kama wewe mwenyewe haujaweka mwanasheria. Unataka mahakama ikuwekee?
 
Anafanya shughuli gani huko london?!
Mara nyingi ana dili na wasanii ndio anawaleta akina fally,mahombi kushirikiana na kusaga
Hizi kiki zimezidi.
Km humjui Yasmine utaona kiki
Kik tu Huyo anatafuta....
Mara ebue Mara samata.....
Mwishoni atajifanya ni wakala wa wacheza mpira

Ova
Show ya fally ipupa dar na koffie 'twanga fotoo' ana mkono wake
Huyu ashakuwa mama kiki
Tuko vzr mno sio kiki mfuatile
Huyo chizi masupa staa ,yeye na mboni masimba
 
Mara nyingi ana dili na wasanii ndio anawaleta akina fally,mahombi kushirikiana na kusaga

Km humjui Yasmine utaona kiki

Show ya fally ipupa dar na koffie 'twanga fotoo' ana mkono wake

Tuko vzr mno sio kiki mfuatile
Huyo chizi masupa staa ,yeye na mboni masimba
Mkuu umesema kweli tupu.., kwenye Show ya Fally aliyofanya Bongo alikuwa anataja sana hilo jina ila sikujuwa kuwa huyo ndo Mhusika!
 
Mkuu umesema kweli tupu.., kwenye Show ya Fally aliyofanya Bongo alikuwa anataja sana hilo jina ila sikujuwa kuwa huyo ndo Mhusika!
Namjua Yasmine vzr mno,mno yaani Bonge la mdada mshua,hana noma ,kifupi anajuana karibu na mastaa wote ,Cameroon walipokuja bongo km ulisikia etoo na song walikua wana zurura town ni yy ndio alikua ana watoa out si Cameron tu,hata ivory coast walivyoweka kambi ya muda kwenda WC 2010,alikua nao karibu
 
Back
Top Bottom