Mtasema, usiku mtalala. Wacha tuendeshe soka kama kuku aliyekatwa kichwa

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
HEMED KIVUYO

Kilichotokea uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa Siku ya pambano la Simba na Yanga ingalikuwe Ni nimojawapo ya Nchi za Ulaya, muda huu kinachosambaa mitandaoni Ni barua za kujiuzulu kwa Viongozi wa Wizara ya Michezo wakianza na Waziri mwenyewe.

Na kwa Mashabiki ingalikua Ni Mashabiki kutoka hapo Kenya tu, muda huu mawakili wangekuwa bize kuwasiliana na wateja wao kufungua shauri la madai . Kwanza muda,pili usumbufu,tatu hasara .

Lakini kwakuwa hapa si Ulaya Wala si Kenya, Basi twasubiri baada ya siku chache Viongozi waliyopaswa kujiuzulu watakaa meza moja na viongozi wa pande zote,watajifungia kwenye hoteli kubwa,waandishi wataambiwa tusubirini hapo nje,wataingia saa nne asb watatoka saa nane na lugha moya tu.

"Nikweli tunajua Mashabiki wetu wameumia Sana tunawaomba watulie na Bodi ya ligi inaaangalia namna ya kuweka ratiba upya pambano hilo lifanyike Tena mchana kabisa,"

Na waandishi wetu watauliza maswali mepesi tu ,eehh vipi na sijui mh Waziri Kama utakuwa mgeni rasmi siku hiyo? Huku akitabasam atasema ,..haaa nikweli kabisa. Yatapita.

Acheni mzaha ndu zangu,Anayepaswa kupanga ratiba ya ligi Ni Bodi ya ligi,Anayepaswa kupangua ratiba ya ligi Ni Bodi ya ligi Tena ikiwa na sababu za msingi na matakwa ya Kanuni.

Aliyeoangua ratiba ya Ligi katika mchezo wa Simba dhidi ya Yanga Ni muhusika wa Kanuni? Hapana . Hapa kumevunjwa Kanuni.

Kuna wenye hoja dhaifu mno katika hili. Wanasema eti Wizara ilisogeza mbele kwakuwa wao wanajua zaidi hali ya usalama ndiyo maana waliona Ni afadhali saa moja usiku kuliko saa kumi na moja jioni. Hahaha inachekesha Sana,

Yaani kwenye Giza kuwe na usalama kuliko kwenye mwanga? Yaani maandalizi ya zaidi ya siku 7 yaje yatenguliwe saa tatu kabla yamchezo huku intelejensia ikishindwa kuona hatari hiyo kabla ya siku 1?

Ukiskiza Sana hotuba za Mwalimu Nyerere utajua tofauti ya Ujinga na upumbavu.

Ni dhahiri Kanuni inaweza kutenguliwa na mamlaka ya Nchi Kama Kuna majanga makubwa kwa Nchi. mfano matetemeko,Mafuriko ama Vita.

Vitu vyote hivyo havipo Tanzania (na tuombe yasitokee)

Ipo hoja nyingine dhaifu wakati wa janga la Corona kupanda juu baadhi ya mechi ziliahirishwa.hiyo unaingia katika moja ya majanga ..sasa tunamajanga gani?

Nasema Wizara kwakuwa toka Tff wasema kuwa wamepokea agizo la Wizara,Wizara haijakanusha na sidhani Kama Tff inaweza kuwasingizia Wizara.

Na katika andiko Hilo Tff haijasema Wizara imetoa sababu gani ya kusogeza mbele pambano hilo ( ingawa kikanuni za Soka hawana mamlaka hayo)

Inaonekana sababu za kuahirisha pambano hilo imekuja ghafla , kwakuwa Kama Wizara ilikuwa inafuatilia ilikuwa inajua tarehe 8/5/2021 Kuna pambano la Simba vs Yanga.

Sababu za dhahiri Kama majanga ambayo yangesababisha kuahirishwa hatujayaona .labda Wizara inafahamu zaidi .

Hatua Kama hii inaweza kusababisha situ taharuki Bali hata kugharimu maisha ya watu.

Watu wametoka mikoa mbalimbali nahata nje ya Nchi,walikata tiketi pengine yakurejea kwao siku hiyohiyo..

Wamelipa na viingilio..halafu hawaoni tetemeko,Mafuriko Wala ajali kubwa Kisha wanasikia kauli nyepesi tu ,meshi usiku,mechi hamna" .

Tff imepokea maagizo hayo kwakuwa imetoka katika mamlaka ya Nchi,ingawa walijua wanakosea.

Unajua Tff walikuwa hawana Shaka kwanini?

Ni kwasababu tumeshawasogeza wanasiasa katika soka na kuona wanamlaka ya kuingilia hata upangaji wakanuni za Soka.

Tumeisogeza Serikali katika maamuzi ya Soka kiasi sasa wameona wanaweza kusema timu hii ihamie kushoto hii kulia na hii icheze kule na hii huku .

Kuingilia Soka kwa maana ya kusaidia ,miundombinu fedha nisahihi kabisa kwa Wizara.lakin siyo kiasi cha kusema huyu asicheze kesho acheze leo.

Na Tff hawakuwa na hofu kwakuwa walijua Yanga na Simba wataufyata tu kwakuwa Ni kauli ya Wizara.

Yaani baada ya mechi kuahirishwa nikarudi nikalalaaa nikaota ota ..Mara naota Wizara hii imegawanywa..Mara naota Wizara ya Michezo imebaki yenyewe...ikajaaaa nikaota Waziri wake Ni Sekilojo Chambua ..Naibu wake Masatu na Mwameja..

Nikaota wakati wanaapishwa Rais anawaambia " hii Wizara siyo ya kuwapa watu shukrani hakikisheni mnaongoza kwa weledi kwakuwa ninyi mmecheza Soka.

Ngoja nilale labda ntaota Tena...mtoto wa Malika
 
Washabiki tuhamasishane mechi zinazokuja tugome kuingia uwanjani hapa nazungumzia mechi zinazoandaliwa na tff siyo zile zinazoandaliwa na caf au fifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…