Mtawa anyakua ushindi wa uimbaji -Italia

Mtawa anyakua ushindi wa uimbaji -Italia

gumboot

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
263
Reaction score
93
Mtawa anyakua ushindi wa uimbaji -Italia
140324145116_the_voice_of_italy_512x288_thevoiceofitaly.jpg








Mtawa wa Italia anyakua ushindi


Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo.


Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki shindano la The Voice.


Scuccia aliyeonekana amevalia mavazi yake ya utawa na msalaba shingoni, alijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa kumfikisha katika ushindi huo.


Mtindo wake wa wimbo wa Alicia Keys, kwa jina 'No One', umetizamwa zaidi ya mara milioni 50 katika mtandao wa You Tube tangu auimbe.


Mtawa huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema kuwa aliamua kushiriki mashindano hayo kufuata ushauri wa Papa mtakatifu Francis, kuwa kanisa liwakaribie zaidi watu wa kawaida.


Source:BBC
 
Alivyoshika maiki utadhani kashika koni? Inaonekana ni mzoefu sana wa kushika hicho kifaa ni haki yake kushinda
 
ungetupiamo na ka audioclip..sipati picha vocal yake!!!
 
Back
Top Bottom