SoC02 Mtazamo halisi wa kimaisha

SoC02 Mtazamo halisi wa kimaisha

Stories of Change - 2022 Competition

Matukio Ep

New Member
Joined
Aug 30, 2022
Posts
1
Reaction score
2
Habari, Kwa Majina Naitwa Theophilus Gugaguga. Mbele ya macho yako ni Nakala Fupi tu Ambayo inalenga kubadilisha Maisha Yako kuelekea katika ukuu. Kaa Chonjo, ukifuatilia kila Neno la Mawazo haya.

Maisha ya Binadamu yamejawa na simulizi Nyingi Sana za Kuchekesha, Kufurahisha, kuhuzunisha, na za kuchukiza. Watu huwa na mitazamo Mbalimbali ya Maisha, Uhai ni Zawadi Pendwa kwa Baaadhi, Lakini ni Gumzo la kusikitisha kwa Wengine, kiasi cha kutamani kujitoa uhai. Ni kweli Kuwa watu huzaliwa Katika hali kadha wa kadha za Kimaisha. Je, Kuna uwezekano wa kuishi na Kufurahia Mema ya Nchi. Kama Kweli Mungu Anatawala na Kusimamia Ulimwengu Wote, Basi Kwa Jinsi Mambo yaendavyo, Mtu anaweza kudhani kuwa Mungu Ameishindwa kazi hii. Basi Ndugu Yangu, Huu Ni Wakati Wa kuyaweka Mambo Wazi Kuhusu Maisha yako.

Mungu MwenyeEnzi na Mwenye Nguvu, Aliumba Dunia na Vyote vilivyomo na akaona kwamba kila alichokiumba ni chema, kisha Akamleta Mwanadamu ili Aitawale. Lakini Pia Maandiko Matakatifu Yanatuambia kwamba, Nchi Imejaa Mema. Hivyo, Mazingira Yetu yameumbwa kiasi kwamba yanaweza kumudu kila Mmoja. Kila Mmoja anaweza kuwa Tajiri, Kila Mmoja anaweza kuwa msomi, kila mmoja anaweza kula chakula Kizuri, Kila mmoja anaweza kujali Familia Yake, Bila Kuzozana Kwasababu ya Uchache wa Rasilimali.

Kuzaliwa katika Familia Maskini, Sio Kosa lako, Lakini Kufa Maskini utastahili Lawama Zote. Vitu Muhimu kuliko Vyote Ambavyo kila mwanadamu huvipata au kuvipokea Katika Maisha yake, ijapokuwa wengi huvichezea ovyo bila kujua, ni muda Na Nafasi. Kama nilivyosema hapo Awali, Hakuna Mtu Aliezaliwa bahati Mbaya, Kuna Nafasi Kwaajili Yako Ulimwenguni. Utakubaliana Nami Nikisema, Haujazaliwa ili ubaki kama ulivyo. Umezaliwa ili uwe tofauti inayotakiwa katika jamii. Hebu Tuangalie Basi Mtu anawezaje kuboresha Maisha Yake.

Watu Wengi Wamelelewa katika Mazingira hatarishi na Yenye Sumu Kali Sana. Nakumbuka Nikiwa Kijana Mdogo Katika Kijiji Cha Kifaru Nilipokuwa nikiishi na Wazazi wangu. Katika Kijiji Chetu, Tuliishi kwenye Nyumba Za Udongo, Hakukuwa na Mtu yeyote aliemiliki Chombo chochote cha usafiri. Lakini Kitongoji Chetu kilipakana na Barabara ya Rami. Mara kwa Mara Magari Hupita na Mara chache Watu Hutembelea Kijiji Chetu. Mara kwa Mara, Mama Alikuwa Akiniambia Kuwa Sisi ni Maskini, na Kamwe hatutakiwi Kucheza na Wale aliowaita Matajiri. Nilikua Katika Mtazamo Wa kwamba Sisi ni Maskini na Sina Kamwe Sitoweza kuwa Tajiri. Familia Nyingi hukuza Watoto Wao Katika Mitazamo isiyo Sahihi Katika Maisha yao. Matokeo Yake ni Kwamba, Watoto Pia Huishi Nayo Maisha yao yote.

1663181701436.png

Kitu cha Kwanza Ambacho Lazima kibadilike ni Mtazamo wako Juu ya Maisha Yako ("ATTITUDE"). Siku zote huwa ni Swala la Muda Tu. Amua Kubadilisha Mtazamo Wako. Amua kuwa na Mtazamo Chanya juu ya Maisha yako. Pengine Wewe ni Muandishi Mzuri, Mtunzi Mzuri, Muimbaji Mzuri au Mwalimu Mzuri. Lakini inawezekana Haujafanya chochote Hadi Leo. Badilisha mtazamo wako, Dunia ina nafasi Kwaajili yako Pia. Pengine Umekuwa ukisubiria Serikali, Au Bahati kutoka Kusikojulikana, Chukua hatua.

Janga kubwa kuliko Yote Duniani ni Janga la Ubinafsi au Umimi ("SELFISHNESS"). Katika Mipango ya watu Wengi, Wanachokifikiria ni Wao wenyewe tu. Ngoja nikupe Chemsha Bongo. Mimi ni Mfanyabiashara hapa Nchini. Nimefanikiwa kuwa na Matawi mikoa mbalimbali. Basi Tawi la Morogoro linakua kwa kasi, na kuleta kipato Kikubwa. Lakini Kilimanjaro Wanadorora. Katika Bajeti yangu, unafikiri ni yupi atapewa Pesa za kutosha, kuendesha na kuboresha Biashara? Mungu Pia Ni Mwekezaji. Kama Wewe ni Mbinafsi usitegemee kumwagikiwa na zaidi ya Kinachokutosha. Ni vyema Apewe Mtu Ambaye atasababisha Maisha ya Wengine yasheheni Furaha, Amani na Upendo. Ubinafsi ni Hatua Mbaya sana ya Maisha. Usijishushe Hadhi ya Maisha yako kwa Kuwa Mbinafsi. Wafikirie Watu wengine, Wajali watu Wengine, Sababisha Tabasamu kwenye nyuso za Wengine kwani, Aliye Mkuu kuliko wote Lazima awe mtumishi wa wote.


1663181341178.jpeg



Watu hufanikiwa pale ambapo wameweza kutatua Matatizo yanayoizunguka Jamii. Ukweli Ni Kwamba Kuna watu Wengi, Pengine Wenye vigezo na ujuzi kama wako. Lakini Sikuzote Dhihirisha, Kuwa wewe ni wa tofauti, kwa Sifa na kwa Uhodari. Epuka Kulalamika pasipo Sababu yoyote ya Msingi. Jifunze kuvaa uhusika Juu ya Kile unachokifanya, Hii ndo maana ya Utuuzima. Hebu Ngoja Nikushtue kidogo Rafiki Yangu. Maana halisi ya kuwa kijana ipo ndani yako . Kijana ni yule Ambaye Bado amebeba Maono, na Matumaini juu ya Maisha Yake, Na wala Si Wingi wa Mvi Kichwani tu, kama Wengi wanavyofikiri. Vijana wengi huishi Kama Wazee Bila Kujua. Wamekubali kuziua Ndoto Zao Na Malengo yao. Usikubali Kuishi Bila Muelekeo, Kila mmoja ana dhumuni la Kutimiza, ujue Mwelekeo Wako Mapema, Na uanze kufanyia Kazi.

Tafakari hii Ikusaidie Kuelewa Pia, Sio kila mlango ulio wazi ni kwaajili yako Kupita. Maisha yenye Fursa Nyingi Sana ni Maisha hatarishi Sana. Kwasababu Pasi Hekima, Unashindwa kufanya Maamuzi Sahihi juu ya Maisha yako. Hakuna Muda utakao weza kuurejesha Tena, Pindi ukishapotea. Wahenga Wanasema Mbio ni Nzuri, Lakini Ziwe Kwenye Muelekeo Sahihi. Njia Usiyoipitia, huna haja ya kujaribisha, Tembea na Yule aliyepita njia hiyo. Ni Muhimu Kumsikiliza Mshauri("Mentor") katika Maisha yako.
1663181293263.jpeg


Hekima Haipatikani kwa kuishi Muda mrefu Duniani. Usipobadili Mtazamo Wako, Basi Hata Ukila Chumvi Nyingi, Utaendelea Kuonesha Dhahiri, Kile kilicho Ndani. Maandiko Matakatifu yanasema ulinde Moyo wako kwa weledi wote, kwa maana Mambo yote ya Maisha ya Mwanadamu yapo Moyoni.

Mungu Halengi kukupa vitu vya kumiliki. Bali analenga kukujenga ili uweze Kumudu Mazingira Yako. Mwanafalsafa Mmoja Alisema, Fanyia kazi Utu wako na Sio umiliki wako. kwa maana Utamiliki Kulingana na Utu wako.

Mwisho, Maneno Yangu Hayatoshi Kuelezea Ajabu za Mungu Wetu. Mungu Aliyeziumba mbingu na nchi, na sisi sote. Yeye Atupendaye kupita kiasi na Aliyetubariki na kuturehemu. Kama Ambavyo Samaki Hawezi kuishi Nje ya Maji, Basi Ndivyo tulivyo. Hatuwezi kuishi Tukiwa Mbali Na Mungu Wetu. Kwa Sala zote na Dua Zote, tusiache kumtafuta na akaonekane Kwetu. Nakutakia Heri katiKa Utekelezaji

Wako, Theophilus.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom