loyan20
Member
- Oct 16, 2014
- 29
- 18
Habari Great Thinkers,
Nimependa kushare na nyie mtazamo wangu kuhusu movies na series za siku hizi toka kwa wazungu.
Nimekuwa nikishangazwa sana na movies hizi ambazo kwa ujumla stori yake inaweza kuwa nzuri tu lakini baadhi ya wahusika wamekuwa wakioneshwa wakijihusisha moja kwa moja na masuala ya ushoga au usagaji! Tena unakuta ni wahusika muhimu wanaofanya yao yakaenda.
Je,kuna nini nyuma ya haya yote? Hivi sio mpango ili tuyaone mambo haya kuwa ni ya kawaida tu? Sio mpango wao kutuonesha mtu anaweza kuwa na matendo haya machafu na akafanya mambo makubwa tu kwenye jamii? Wanatumia characters(wahusika) wenye mvuto mkubwa kwenye hiyo "story" ili kuiaminisha dunia kuwa hayo ni mambo ya kawaida tu, yaani mtu yeyote anaweza akawa "gay" na maisha yakaenda kama kawaida.
Je, wanataka kutufundisha nini? Ushoga ni LAANA kubwa kwa MUNGU ni jambo lisilotakiwa kabisa hata na tamaduni zetu za kiafrica. Watoto wetu wanajifunza nini kutoka kwenye filamu hizi? Tunajenga jamii ya sasa na ya badaye yenye mtazamo upi?
Kwa hali ya kawaida kile tunachokiona na kukisikia huathiri moja kwa moja fikra zetu na mitazamo yetu kisha tabia zetu. Mtakumbuka zamani ilikuwa ni jambo la ajabu tena la aibu kuona watu wakikiss hadharani lakini sasa ni jambo la kawaida tu, haya yote ni baada ya mitazamo yetu kubadilishwa taratibu na kile tunachokitazama.
Mtakuwa mashahidi zangu kwa series/movies kama Orphan Black, Empire, Sense 8, etc.. baadhi ya wahusika wake wamejihusisha na mambo haya maovu tena yanaoneshwa wazi wazi.
Hii ni hatari kubwa katika maadili ya jamii yetu ya sasa na ya badae. Kama tukikubali kubadili mitazamo yetu kwa kutazama mambo haya machafu, tutawezaje kuyapinga?
Hebu tuwe makini sana na kile tunachochagua kukitazama ama kukisikia. Zaidi tuwe makini na kile kinachotazamwa majumbani na watoto/wadogo au ndugu zetu.