Mtazamo: Hollywood movies na suala la ushoga!

loyan20

Member
Joined
Oct 16, 2014
Posts
29
Reaction score
18
Habari Great Thinkers,

Nimependa kushare na nyie mtazamo wangu kuhusu movies na series za siku hizi toka kwa wazungu.

Nimekuwa nikishangazwa sana na movies hizi ambazo kwa ujumla stori yake inaweza kuwa nzuri tu lakini baadhi ya wahusika wamekuwa wakioneshwa wakijihusisha moja kwa moja na masuala ya ushoga au usagaji! Tena unakuta ni wahusika muhimu wanaofanya yao yakaenda.

Je,kuna nini nyuma ya haya yote? Hivi sio mpango ili tuyaone mambo haya kuwa ni ya kawaida tu? Sio mpango wao kutuonesha mtu anaweza kuwa na matendo haya machafu na akafanya mambo makubwa tu kwenye jamii? Wanatumia characters(wahusika) wenye mvuto mkubwa kwenye hiyo "story" ili kuiaminisha dunia kuwa hayo ni mambo ya kawaida tu, yaani mtu yeyote anaweza akawa "gay" na maisha yakaenda kama kawaida.

Je, wanataka kutufundisha nini? Ushoga ni LAANA kubwa kwa MUNGU ni jambo lisilotakiwa kabisa hata na tamaduni zetu za kiafrica. Watoto wetu wanajifunza nini kutoka kwenye filamu hizi? Tunajenga jamii ya sasa na ya badaye yenye mtazamo upi?

Kwa hali ya kawaida kile tunachokiona na kukisikia huathiri moja kwa moja fikra zetu na mitazamo yetu kisha tabia zetu. Mtakumbuka zamani ilikuwa ni jambo la ajabu tena la aibu kuona watu wakikiss hadharani lakini sasa ni jambo la kawaida tu, haya yote ni baada ya mitazamo yetu kubadilishwa taratibu na kile tunachokitazama.

Mtakuwa mashahidi zangu kwa series/movies kama Orphan Black, Empire, Sense 8, etc.. baadhi ya wahusika wake wamejihusisha na mambo haya maovu tena yanaoneshwa wazi wazi.

Hii ni hatari kubwa katika maadili ya jamii yetu ya sasa na ya badae. Kama tukikubali kubadili mitazamo yetu kwa kutazama mambo haya machafu, tutawezaje kuyapinga?

Hebu tuwe makini sana na kile tunachochagua kukitazama ama kukisikia. Zaidi tuwe makini na kile kinachotazamwa majumbani na watoto/wadogo au ndugu zetu.
 
Ukistaajabu ya ushoga naomba usishangae series mpya inayokuja inaitwa lucifer..Yaani shetani maisha ya kuzimu yamemchosha akajiuzulu na kuja ishi dunian kwenye mji wa angels ( los Angeles) jamaa wanafika kiwango cha mwisho cha kukufuru.
 
Well said, kwa mfano Scandal ya Olivier Pop, chief of staff wa WHITE HOUSE ni gay halafu eti anapiga mzgo kama kawaida as a right hand of the President, can u imagine??
 
Zinachefua sana, nyingine series ya Ophan Black.
 
People are coming out like WTF..
 

Attachments

  • 1441431855218.jpg
    42.7 KB · Views: 873
Mimi ndio maana nikiwa na muda naangalia za Kikorea tu tena za vijijini.

Hizo zimeshanishinda zinatia aibu watu wanavuana nguo tena wa jinsia moja..kama umekaa na familia ndio kabisaa.
 
Wazungu wameona kutulazimisha kuruhusu kikatiba kwa ushoga itachukua muda mrefu sana so they came with another strategy
Wanajua sisi ni watu wa kugeza sana tunavyoviona kwenye muvi zako pia tunazipenda sana
So what they do ni kuweka kitu kwenye mind yako kuwa ushoga na usagaji ni kitu cha kawaida coz utakuwa wakiona kwa kila muvi utakayokuwa waangalia
So polepole mind set yetu itakubaliana na hilo jambo bila hata ya kupitisha bungeni. Kuna siku wakija wakisema tukubali wala hatutapinga tena coz kichwani tushakubali
That's why muvi zao now zina ushoga mwingi mpk zinakera.
Wakishaona kuna seris nzuri inayopendwa wanaingiza na scene za kishoga ilimradi tu
 
Ungejua hata wazungu hawajui kama izo muvi zinaangalia Afrika ndio maana hata afrika sio target market ya movie zao ukitaka kujua hilo hata wewe hujawai kununu movie orginal zaidi ya kudownload torrent..
 
Mpaka kinyaa, nyee!
Sijui tutaangalia nini.
 
Hawa wapumbavu wanataka kuspread hii kitu kijanja ila ni wajibu wetu kua makini ya nini tuige na nini tuignore Mungu atutangulie la sivyo hii dunia inakuja kua kitu cha ajabu sana
 
Ungejua hata wazungu hawajui kama izo muvi zinaangalia Afrika ndio maana hata afrika sio target market ya movie zao ukitaka kujua hilo hata wewe hujawai kununu movie orginal zaidi ya kudownload torrent..

haha wewe unafurahisha nani kakwambia Africa sio target yao? ndio maana unaambiwa dunia imekua kama kijiji. Kila kitu kipo on your fingertip. Ni dhumuni lao Africa tuipate does not matter una download ama unafanyaje
 
Sidhani kama ukiangalia inakufanya ugeuke kuwa shoga.
 
Ushauri wangu usipende kuwafutafuata hao wazungu.angalia movie za nyumbani.wale wana tamaduni zao.hujalazimishwa kuangalia series zao
 
Mpaka ume_post hapa ina maana message imefika kwa mlengwa ambaye ni wewe, so hao wakollon i (wazungu) wanajua wanachoki fanya nyuma ya pazia.

-TAKE CARE.
 
Ukistaajabu ya ushoga naomba usishangae series mpya inayokuja inaitwa lucifer..Yaani shetani maisha ya kuzimu yamemchosha akajiuzulu na kuja ishi dunian kwenye mji wa angels ( los Angeles) jamaa wanafika kiwango cha mwisho cha kukufuru.

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ very comic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…