Unapojaribu kuomba msaada sehemu yoyote katika jamii uishiyo,
Si vyema ukasimama mbele ya watu na kuomba msaada mtu kwa kutamka jina lake unaweza jijengea au kujitengeneza balaa fulani la kukosa msaada unaoeleweka kabisa. Kama unaona hamna anayeweza kukusaidia mfuate mtu unayemwamini kwa Siri (faragha). Kuliko kumexpose mtu wazi wazi.
Mfano:
Unahitaji msaada na unamfahamu mtu anayeweza kukusaidia mfuate mmalizane mkiwa peke yenu.
Lakini unaweza jenga picha, ya kwamba unapoomba msaada mtu katikati ya watu usio wajua Nini hutokea kwa wale usio wajua hata kikiwa ni hasi au chanya?
Je siku mtu huyu akikosekana utamsubiri mpaka arudi kutatua shida yako?
Vipi kama hatokuwa na msaada huo utawafuata wale ambao haukuona kuwa wana msaada kwako hapo hawali?
Hii si kwa Waafrika tu hata kwa wasiokuwa Waafrika. Ninachotaka kukuonyesha ni kutowapa watu kipaumbele au kuwasifia katikati ya watu wengine mara kwa mara na wakati huo huo haufahamu kuwa Kuna wanaoweza kukupa msaada zaidi ya hapo ila huwatambui kwa sababu umekalili watu.
Kumbuka kuwa jamii sio taasisi yaani katika jamii ni ngumu kufahamu uwezo wa mtu kirahisi katika jambo fulani ila kwenye taasisi ni rahisi.