Mtazamo: Kupoteza kwa Simba SC dhidi ya Azam FC, Ahmedy Ally kachangia kwa asilimia kubwa sana

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kabla ya mchezo niliandika uzi ulisema Azam atashinda au atadroo mbele ya simba sc na kweli ikawa hivyo.

Tatizo lilianzia kwa Ahmedy Ally baada ya kuzungumza maneno yakukatisha tamaa/kukata tamaa pale simba ilipotoa droo dhidi ya namungo. Kwa sisi tuliocheza mpira tunajua ili timu ipate matokeo /ifanye vizuri uwanjani huwa vinazingatiwa vitu viwili ama vitatu muhimu.

1/ Saikolojia ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwa ujumla.
2/ Body fitness ya wachezaji

Hivyo ni vitu muhimu sana Tena sana katika ulimwengu wa football.

Gemu ya Jana wachezaji waliingia kutimiza ratiba lakini kisaikolojia walikua hawapo sawa kabisa na hiyo ni sumu ilitoka kwa Ahmedy Ali kuzungumza maneno yakukatisha tamaa, ni Bora ahmedy Ally angezungumza kauli zake zile zile za kutia moyo Kama anavyozungumza kuliko kutoa kauli ambazo moja kwa moja ziliiathiri benchi la ufundi mpaka wachezaji na kujikuta wanakwenda kutimiza ratiba tu.

Tazama mzamiru, mohammedi Hussein, shomari kapombe.

Hawa ni wachezaji amabao huwa Wana morali wakati wote lakini gemu ya Jana walikua Kama hawapo kabisa ndani ya pitch.

My take, wasemaji wa timu muangalie maneno mtakayozungumza kabla ya mchezo au baada ya mchezo yataleta impact gani?

Neno dogo linaweza kuleta effect kubwa sana kuliko ulivyozania.
 
Huyo Bw. Ahmed aliwavimbisha vichwa wachezaji wakawa vichaa sasa wamepigwa na vitu vizito vichwani na kushika adabu zao.

Hawana hata kikombe kidogo cha kunywea kahawa msimu huu!
 
Hivi tangu lini Ahmed Ally msemaji wa Simba SC amekuwa akiingia uwanjani kucheza?

Jana tumefungwa kwa kuwa Wenzetu Azam walikuwa bora kwenye kutumia nafasi chache walizopata kutuzidi lakini sio kwasababu ya huyo Msemaji
 
Broo umeangalia mpira vizuri??
Umetazama namna gani Wana Simba walivyojikanyaga mzee

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hivi tangu lini Ahmed Ally msemaji wa Simba SC amekuwa akiingia uwanjani kucheza?

Jana tumefungwa kwa kuwa Wenzetu Azam walikuwa bora kwenye kutumia nafasi chache walizopata kutuzidi lakini sio kwasababu ya huyo Msemaji
Robertinio anaingia uwanjani?
 
Kuna utofauti wa Msemaji na Kocha.

Kocha ana taaluma na mbinu za kujua nani acheze wapi na kwanini
Msemaji ni loudspeaker ya kocha na uongozi mzima wa timu. Hivyo alichokisema ni maoni ya kocha na wala Robertinio hajakanusha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…