Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mkuu huo ni ukweli mchungu sana umeusema. Wapo watakaokutukana lakini umesema kweli kabsa. Ndio maana hatusogei popote. Subiria mawe sasa.Baada ya uchunguzi wangu wa muda mrefu nimebaini jambo hilo, kwamba wachezaji wengi wa soka wa nchini Tanzania wala hawakuwa na ndoto hiyo bali wengi wameingia huko kama Plan B. Na ni baada ya kushindwa maisha ama kufeli masomo.
Kwa mfano katika maeneo ambayo elimu ni kipaumbele cha kwanza kwa watoto, Upanga, Masaki, Oysterbay au Mikocheni hakujawahi kuzalisha wanasoka.
Lengo la andiko hili si kuponda wanasoka wetu , bali ni kuanzisha mjadala wa kujua kisa cha kutothaminiwa kwa mpira wetu kiasi cha kuwafanya wazazi wakwepe kuwaingiza watoto wao.
Nini kifanyike ili soka iweze kuvutia kila mmoja na ionekane kama chanzo halali cha ajira ?
Tena hiyo zamani unayoisema ndio kipindi pekee ambacho wanasoka wa Tanzania walikuwa wasomi , maana wengi waliibukia umiseta , kumbuka kwamba hivi sasa vipaji vinatokana na ndondo cup .Mtoa hoja umechemka,usizungumze tu kwa story za vijiwen,lig kuu ya tanzania kuna wachezaj kibao wana jiwe la kwanza,na baadh nawafaham wamemaliza masters,mfano kipa wa toto /nadhan baadae alienda tim ya mbao,ana MA yule jamaa,ungezungumza kuhusu wale wa zaman angalau,ila sema nao fursa za shule ziliwabana maana zilikua chache au uduni wa maisha,ila baadae walivyopata cent wakapiga shule vizur tu,mfano leodeger Tenga,tatizo lenu vijana wa leo mkipata hivyo videgree vyenu mnahis nyie ndio wasomii
Wanaelimu za academ boraa kabisaa walizofundishwa toka utotoo..mamboo ya elimu hususan ya bongoo n nyokooo ..wakina boko hana elimu lkn msakuzi kule wameshajiwekezaa vya kutoshaa na maishaa yanaendeleaa ...maisha n ww jinsi utakavyoweza kupambana nayo ..Hivi Pele, Maradona, Messi, CR7, Zidane, De Lima, Ronaldinho, Figo. Wanaelimu gani?
Mimi naishi Tandika Mwembeyanga .Japo naona kama unajichanganya mwenyewe kwenye mada yako, lakini tuanzie hapa: Ushawahi kuishi Upanga, Masaki, Oysterbay au Mikocheni?
Soccer ni mchezo wa watu masikini ambao ndio huwa wanaona ni njia pekee itakayo wasaidia kutoka kimaishaa maana kwao kupata elimu bora ni mtihani wengi huishia kufanya kazi zile za mwisho kama udereva, kufanya usafi, kulinda mifugo, kuuza maduka, kusafisha viatu.. Na matajir wao huwa wanafocus kuwaandalia mazingira mazuri ya badae watoto wao ndio maana huwapeleka shulee nzuri na badae kuja kuwa viongozi wakubwa wa serikali na makampuni makubwa... Ndio maana hata ukiona kina Pele, messi, Ronaldo, Ronaldinho.. N. K wakaamua kuwekeza nguvu zao kwenye [emoji460] na hata familia zao zilikua radhi kuwaachia maana zilijua shule haita wafikisha mbalii bora mungu amewajaalia vipaji na ametokea mtu wa kuviendeleza basi haina neno. Hata athletes wakubwa wote duniani hawana shulee angalia NBA na michezo mingine. Hivyoo michezo ni kimbilio la watu maskinii kama vile matajiri wanavyoshindana kwenye shuleeSoka ni mchezo wa watu masikini (kwa wachezaji) na ni wa watu matajiri (kwa mashabiki na wamiliki wa timu)
Hii ipo hata ulaya, chukulia mfano wa A.Sanchez.. Pia kuna matajiri waliolazimisha chukulia mfano Beckham.
Asante kwa ushahidi .Soka ni mchezo wa Maumivu sio bongo tu,Angalia ata mastaa wa Dunia wa Soka,Mazoezi asubuhi, jioni,kuumizwa,kuvunjika,kutukanwa na mashabiki na kupigwa pia, Watoto wengi wa kishua hawana moyo huo wa kupambana wana alternative nyingi za maisha.
Unasubiri nini ?Nasubiria kwanza
Huku kwetu Tandika MwembeYanga mzazi anaweza kumuachisha mtoto shule ili akacheze mpira , je huko kwingine mzazi anaweza kukubali ujinga huo ?Kwanza aliokwambia waliokulia Upanga na Mikocheni ndio wasomi nani? Tuliokulia na kusoma Dar ndio tunaujua ukweli, kuna watoto wa Masaki kibao wanakwenda shule alimradi tu.
Huku kwetu Tandika MwembeYanga mzazi anaweza kumuachisha mtoto shule ili akacheze mpira , je huko kwingine mzazi anaweza kukubali ujinga huo ?
Kwani mtu huitwa msomi akifikia ngazi ipi ya elimu? Tuanzie hapa kwanza.Baada ya uchunguzi wangu wa muda mrefu nimebaini jambo hilo, kwamba wachezaji wengi wa soka wa nchini Tanzania wala hawakuwa na ndoto hiyo bali wengi wameingia huko kama Plan B. Na ni baada ya kushindwa maisha ama kufeli masomo.
Kwa mfano katika maeneo ambayo elimu ni kipaumbele cha kwanza kwa watoto, Upanga, Masaki, Oysterbay au Mikocheni hakujawahi kuzalisha wanasoka.
Lengo la andiko hili si kuponda wanasoka wetu , bali ni kuanzisha mjadala wa kujua kisa cha kutothaminiwa kwa mpira wetu kiasi cha kuwafanya wazazi wakwepe kuwaingiza watoto wao.
Nini kifanyike ili soka iweze kuvutia kila mmoja na ionekane kama chanzo halali cha ajira ?