Uchaguzi 2020 Mtazamo: Tunakoenda watu watakuwa tayari kujitokeza na kuitikia wito wa maandamano ya amani kuliko kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwa yanayoendelea,wananchi wanapata picha kuwa hakuna tena uchaguzi na hivyo hakuna maana yoyote ya kushiriki mikutano ya kampeni kwani hakuna tena kinachoitwa uchaguzi kwa maana ya uchaguzi kwa sifa zake.

Hivyo, wananchi hawa wataamasika zaidi kuitikia wito wa maandamano ya amani kuliko kwenda kwenye mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa kwasababu mpaka sasa mikutano hii imeshapoteza maana kutokana na idadi kubwa ya wagombea wa upinzani katika ngazi zote isipokuwa uraisi kuenguliwa, huku zoezi hilo likionekana kuendelea licha ya muda wa kufanya hivyo kisheria kuwa umepita.

Wananchi hawatakuwa na hamasa ya kuhudhuria mikutano ya kampeni bali mioyo yao itaguswa zaidu na wito wa kuandamana kwa amani kudai uchaguzi ulio huru na wa haki na kudai wagombea wa upinzani walioenguliwa warudishwe.

Kwa mtazamo wangu,huku ndiko tunakoelekea kutoka na ukweli kuwa mpaka sasa swala la uchaguzi limeshapoteza maana na hamasa miongoni mwa wananchi.
 
Vipi mmeandamana leo?., Wabunge mnalipwa milioni 12 kwa mwezi na marupurupu kibao na hamkumbukagi mnakotoka nani wa kuandamana apigwe kwa ajili yenu?.. Huwa sielewi nani anawadanganya upinzani mnakubalika kwa wananchi.

Watanzania ni watu tofauti na mnavyodhani. Waweza kuongea pumba wakashangilia Ila siku ya kuandamana huwaoni. Yote aliyofanya JPM yanaonekana nyie endeleeni kupiga kelele mitandaoni, mtaandamana kwenye Keyboards tu na vi smart phone vyenu.
 
Ngoja tusubiri tume watoe majibu ya rufaa wakileta ubabaishaji tunaingiza raiya rodini kwa amani.
 
Hakuna kitu, iahatoka hiyo! Twende kawe tukasikilize sera
 
Ngoja tusubiri tume watoe majibu ya rufaa wakileta ubabaishaji tunaingiza raiya rodini kwa amani.
Mnasubiri majibu gani wakati jana lissu kasema maandamano yanaanza leo? Au hujui kuwa tune imeshatangaza majina ya wabunge 18 wamepita bila kupingwa.
 
Pamoja na kulipwa hiyo mil 12 bado wanataka kutuchangisha fedha. Mwaka huu hatutakubali kuchangaboesa yoyote
 
Go ahead mbona ishatolewa jana kuwa maandamano yanaanza leo? Au hukuelewa?
 
Chadema tuliwaonya humu kua siasa za uzushi,chuki na kupinga kila jambo hazitawajenga kwa muda mrefu. Jana mumeanza kuipata kali ya uchaguzi.

Maandamano alishindwa mange, ukashindwa ukuta, sijui munajipya gani. Bungeni mhe msigwa alipata kusema maana ya neno insanity.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…