KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Habari za muda huu waungwana.....
Mimi nadhani maisha ya kiumbe mwanadamu hapa duniani yamekuja mfano wa simu iliyojaa chaji na kutolewa kwenye chaji pindi anapozaliwa kutoka tumboni kwa mama yake.......
Na chaji hutumika na kupungua kwa kadri anavyoziiishi nyakati zake hapa duniani.....na bahati mbaya hakuna kuongeza chaji badala ni kutumia chaji...
Kwa muktadha huo ni kuwa iko siku chaji itaisha na kuzimika kwa kadri mola wake alivyo mkadiria......
Kiuhalisia ni kuwa kwa kadri unavyoziishi nyakati zako ndivyo unavyozikaribia siku za agano lako na mola wako za kuishi juu ya mgongo wa ardhi.......
Hekima ni kuwa kila inapokupita nyakati unatakiwa kukaa na kutafakari ya nyuma na kuyarekebisha huku ukiziishi vyema nyakati zijazo ili kuwa na mwisho mwema........
Muungwana hawezi kushangilia kuisha kwa chaji kwenye simu yake hali ya kuwa hana uwezo wa kupata chaji nyingine bali hutafakari na kuitumia vyema chaji kidogo iliyobakia ambayo pia inaendelea kuisha.......
Tujitahidi kuziishi nyakati zetu vyema kwa kadri tulivyobarikiwa huku tukijua kuwa iko siku chaji yetu itakwisha na tutazima(kufariki).......
Hata tuliowazika nao walikuwa watu kama sisi, wenye mipango na mikakati kama sisi na pengine hawakuwa wanajua kuwa wanaziishi nyakati zao za mwisho kwani umauti huja ghafla......
Najua taarifa hii inaweza isiwe ya kupendeza kwa watu walio wengi lakini wanadamu ni vyema kukumbushana kwani kujisahau ni maumbile yetu.......
Nawasilisha......