Hata wamfukuze si bado ndio atazidi kuwachora,kitu kimoja nikuwa GADO hamuogopi mtu ,alikuwa anamchor baba Moi enzi hizo sembuse iwe hawa akina ''Nusu Mkate''pia ikumbukwe GADO anatoka kabila la watu ambao kusema spade ni kijiko kwao ni mwiko ,wakati wote husema yale wanayoyaamini,GADO ni Mnyakyusa kutoka mkoa wa Mbeya,na kwa Watanzania watu wa mkoa wa Mbeya wanajulikana kuwa wazi na wasiohofia lolote ndio akina Mwakyembe,akina Ulimboka.Na hao ni wajukuu wa wazee wa kinyakyusa ambao hata Mwl Nyerere alikuwa anawaheshimu.Hata raisi wetu wa Tanzania aliye madarakani anawajua watu wa Mbeya,huyo GADO hata prezidaa wetu ameahi kumchora na wapambe walipiga kelele wee hadi wenyewe wakafyata,kwa kifupi GADO hanyimwi usingizi hata kidogo na akina UhuRuto.