Pre GE2025 Mtazamo wangu: Akigombea na kushinda urais 2025 ataiacha CCM hoi sana 2030 kuliko ilivyokuwa kwa Rais yeyote aliyemtangulia!

Pre GE2025 Mtazamo wangu: Akigombea na kushinda urais 2025 ataiacha CCM hoi sana 2030 kuliko ilivyokuwa kwa Rais yeyote aliyemtangulia!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Hii ni fact kutokana na uzoefu wa mahali pengi duniani na hata ccm kwenyewe huwa rais anapotumikia muhula wake wa mwisho ni kipindi kigumu sana kiuongozi.

Kuna kuwa na mambo mengi sana yamemchosha hivyo hata yeye mwenyewe huona amalize tu ngwe yake akapumzike awaachie wengine waendelee.

Kunakuwa na kakisirani fulani hivi hasa kwa wapenda madaraka kuona ndo cheo kinamponyoka na hana namna ya kukiretain hivyo hufanya bora liende.

Kuna magenge ya wajanja wa mjini kwa kuwa wanajua anamalizia na akili imechoka wanamchomekea vitu vingi na kumwingiza kingi ili wapige hela.

Makundi ya wanaotaka urais huanza kuumizana ili kupigania nafasi. Makundi haya huwa na nguvu sana kiasi kwamba yahitajika nguvu ya ziada kutuliza mambo

Hizi ni baadhi tu ya sababu zinazofanya muhula wa mwisho wa urais liwe jambo gumu sana kwa chama.
Ni katika mazingira hayo huhitajika mwenyekiti tough sana na anayesikilizwa si kwa sababa ya majeshi au uamiri jeshi, bali awe amejaaliwa hivyo.
Ilikuwa nafuu kama angeachia sasa kwa sababu kwanza kuna wasiwasi na pili waliojopanga bado hawajakita mizizi sana wanadhibitika kirahisi.

Nashauri aweke mpira kwapani aachie vijana waendelee na mtanange atalinda heshima

Maana nakumbuka yule wa msoga manusura chama kimfie. Kama mama akikomaa kugombea.... watch out part two is loading.
 
Hadi sasa hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kuitikisa CCM. Vyama vyote vya upinzani ni dhaifu sana.
Viongozi wote wa vyama vya upinzani wanajali maslahi yao binafsi, ubinafsi, umimi, wamegeuza vyama kama taasisi zao/ sacos.
 
Hapa tunazungumzia ccm na maswahibu yake hao wapinzani tutaweka mada yao
 
Hadi sasa hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kuitikisa CCM. Vyama vyote vya upinzani ni dhaifu sana.
Viongozi wote wa vyama vya upinzani wanajali maslahi yao binafsi, ubinafsi, umimi, wamegeuza vyama kama taasisi zao/ sacos.
Umemaliza kila kitu
 
Umemaliza kila kitu
Hapana kwa habari ya upinzani magonjwa yake yanajulikana ila ndani ya ccm kuna wingu zito sana hufunika kuelekea kupata mgombea mpya na hapa ndipo huhitajika mtu mwenye ushawishi wa kutuliza hali
Rejea wakati wa Mkapa-Nyerere wakati wa kikwete - yeye mwenyewe alijitengenezea limtandao hivyo haikuwa ngumu sana, wakati wa Magu- Mkapa ndiye alinusuru jahazi na sasa.....
 
Pona ya Tanzania thidi ya ufisadi na ubathirifu wa mali za umma ni CCM kuwa na Mgombea wa Urais Mwanaume 2025
 
Hadi sasa hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kuitikisa CCM. Vyama vyote vya upinzani ni dhaifu sana.
Viongozi wote wa vyama vya upinzani wanajali maslahi yao binafsi, ubinafsi, umimi, wamegeuza vyama kama taasisi zao/ sacos.
Chama sawa, lakini wananchi ni zaidi ya vyama vya siasa, wananchi wakiwa tayari hakuna wa kuzuia.
 
Wizi na ubadhirufu wa mali ya Umma haukuanza leo na hakuna mtu wala Rais mmoja anaeweza kudhibiti wizi huu
Mnatakiwa kuanzia juu mpaka mawaziri na wakurugenzi wawe aina moja ya kusimamia kwa dhati mali zote na miradi yote
Hapo kidogo mtasogea mbele
La sivyo mtalaumu kila Rais anaepita
Magu alijitahidi lakini nafikiri yeye ndio kapigwa kiliko wengine wote
Wengine walitumia jina lake na kuweka pistol viunoni kusema Rais kasema
Wote tunajua kilichokua kinaendelea
Kwa hiyo na Mama atapita na mtasema
Atakuja mwingine mtapigwa vizuri zaidi na wimbo utakuwa huu huu
 
Hapa hatujadili ni rais gani atakuja kumaliza wizi hoja iliyoko mezani ni kwamba rais akiwa awamu ya mwisho anakuwa kwenye mtego mkubwa sana kwa sababu mazingira ya wakati huo huwa rahisi kutengeneza magenge ya matapeli kwa madhumuni mbali mbali ikiwemo kuchafuliana majina
 
Sasa kama upo uhakika wa kugombea na kushinda, kwann tufanye uchaguzi?
 
Back
Top Bottom