Mtazamo wangu:Bunge Maalum la Katiba limetuonyesha watu muhimu sana katika Taifa Letu

Mtazamo wangu:Bunge Maalum la Katiba limetuonyesha watu muhimu sana katika Taifa Letu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
Wasalam wana JF

Leo ningependa nitoe maoni yangu machache tangu Bunge Maalum la Katiba lianze Februari 18, 2014. Nimefuatilia mijadala michache sana kutokana na kazi yangu kunifanya nisipate muda wa kutazama Bunge kwenye hatua ya utungaji wa kanuni. Nasema Taifa lina hazina kubwa ya watu wenye uelewa mpana na wasio na uroho au umimi wa kutaka kupata umaarufu.
Kwa neno hilo napenda nitambue ujuzi na uelewa wa Mhe Prof Costa Mahalu. Huyu ndiye Mwenyekiti wa kamati ya muda ya kutunga kanuni ambayo kimsingi inamsaidia Mwenyekeiti wa Muda kumshauri juu ya hilo. Kama Prof Mahalu angetaka kupata umaarufu ninaamini kabisa angeweza kuhodhi kujibu maswali yote yanayoibuliwa na wajumbe wa bunge hilo. Kwa nini nasema hivyo? Mfano jana tarehe 6.3.2014 nilibahatika kukuta mwishoni kidogo mjadala wa kanuni hasa za mavazi na lile suala la kama mjumbe ikitokea amefariki nani atabeba gharama za mazishi?

Nimekuwa nikiona swali likiulizwa basi Mwenyekiti wa muda ambae ni Kificho, analipeleka kwa Prof Mahalu. Profesa naye ampa mjumbe wa kamati yeyote yule kujibu swali hilo. Mfano baadhi ya maswali rahisi kabisa angeweza kuyajibu yeye mwenyewe, lakini anaamua tu kumpa mwingine ajibu. Swali la mfano kwangu ni lile la endapo mjumbe wa bunge maalum la katiba akifariki nani atabeba gharama za mazishi? Swali hili Profesa Mahalu aliamua kumsimamisha Tundu Lissu alijibu. Na kwa namna jibu lilivyokuwa rahisi sikutegemea kuwa angempasia Lissu, kwani alikuwa na uwezo wa kujibu yeye mwenyewe. Tundu Lissu kwa madaha kabisa akaanza kutoa somo la kuwa wajumbe wamegawiwa vijitabu vya kanuni. Akashauri wasome. Baada ya hapo akatoa jibu rahisi la kusoma kipengele husika na kukaa chini.

Hapo pia palitufundisha kuwa baadhi ya wajumbe hawa hawsomi vijadilida wanavyopewa. Samahani kama nitakuwa nimekosea. Hawasomi. Laiti mjumbe yule angekuwa amesoma asingeuliza swali lile.

Kuna wajumbe wale 201, baadhi yao wamenivutia sana. Ni wajenzi wazuri sana wa hoja. Natamani sana mwakani wawe wabunge kamili na si kuishia hapa. Wabunge hawa wametoa somo kuwa tuna watu wenye ulewa mpana na wenye roho safi. Wasio na chuki.
Namsifu pia Ezekiel Oluoch ambaye amekuwa maarufu ghafla kwenye bunge hili. Michango yake ya kila mara inaonyesha kuwa yupo makini kusoma vijadilida vya kanuni. Nilitegemea sana wabunge wazoefu na ukumbi huo ndio wawe vinara. Lakini wengi wa wabunge hawa wazoefu wameendeleza yale yale ya uchama. Maria Sarungi naye amekuwa mtoa hoja mzuri sana. Nimewapenda kwa kweli.

Maoni yangu ni kuwa watu jamii ya kina Mahalu, Oluoch na Maria wanapaswa kuingizwa kwenye bunge bila kujali wamechaguliwa au la. na hapa katiba mpya iweke kipengele cha kuteua wabunge wenye tija kwa taifa.

Ni hayo tu wakuu
 
Na mimi nampendekeza Profesa Ibrahim Lipumba awe mbunge wa kudumu maana si mropokaji bali hutumia ujuzi na elimu aliyopata kuchangia hoja kwa nguvu za hoja! kuna baadhi ya wajumbe huwa wananikera hasa kwa kuishiwa na hoja bali hutaka umaarufu kwa kutaka kuchangia kila kitu tena kwa mgongo wa kipengele cha kanuni ya taarifa nk! la kusikitisha baadhi yao hata lugha ya Kiswahili inawapiga chenga sijui waliwezaje kupita ktk mchujo wa kamati za vyama vyao huko majimboni na kuchaguliwa kuwa wabunge!!!!
 
Asante kwa maoni yako. Ila nahofia, naona kama yamekaa kiushabiki hivi. Leo hatumwamini mtu hapa anapoanza kuwataja watu.
Lakini kama nia yako ilikuwa njema, basi natamani Mola awafungue macho wahusika wa majimbo hayo waliko toka wawarudishe bungeni 2015.
As yu have put it on your ID; An empty stomach is not a good adviser. Many of these pro-people here are forced by this enemy; An Empty Stomach. Hii ndo Silaha na Ngao ya CCM. Wameitumia kwa muda mrefu sana sasa na bado wanafanikiwa.
 
Unataka tena Wabunge wa viti maalumu???

Hapana waingie kwa umuhimu wa wanachi. Fahamu kuna watu wengi wazuri kwenye taifa hili lakini hawapiti kwenye mfumo wetu huu wa mizengwe. Lakini wana tija kubwa.
 
Asante kwa maoni yako. Ila nahofia, naona kama yamekaa kiushabiki hivi. Leo hatumwamini mtu hapa anapoanza kuwataja watu.
Lakini kama nia yako ilikuwa njema, basi natamani Mola awafungue macho wahusika wa majimbo hayo waliko toka wawarudishe bungeni 2015.
As yu have put it on your ID; An empty stomach is not a good adviser. Many of these pro-people here are forced by this enemy; An Empty Stomach. Hii ndo Silaha na Ngao ya CCM. Wameitumia kwa muda mrefu sana sasa na bado wanafanikiwa.

Hapana sina ushabiki kwa hili. Nazungumza kutokana na kuguswa na michango yao. Huyu Profesa ndio kwanza namwona kwenye bunge hili ukiachilia mbali kumsikia tu wakati ule wa kesi yake.
 
Back
Top Bottom