Mtazamo wangu dhidi ya TAKUKURU

Mtazamo wangu dhidi ya TAKUKURU

Standards Person

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2021
Posts
672
Reaction score
860
Takukuru ni chombo cha kumulika na kuwaangza watoaji, wala rushwa na hata wanaoishabikia.

Inaonekana kwamba aidha kuna Takukuru ambao wanafanya kazi sana au wengine hawaonekani kufanya kazi kutokana na maeneo kwakua labda hakuna vitendo vya rushwa au hao takukuru wenyewe ni wala rushwa.

Ilitakiwa ifanyike tathmini ya jumla kwa zile ofisi ambazo hasiisaidii serikali kupambana na rushwa basi walengwa waondoke ili wapishe wengine. Kwanamna dunia ilivyo haiwezekani inaisha miezi sita ofisi haijakamata mlarushwa wala mtoa rushwa.

Naikitokea kama nikweli hawajakamata basi itakua wananchi wa eneo husika hawana elimu ihusuyo rushwa. Hivyo bado lawama inarudi Takukuru.

Ninasema hivyo kwani rushwa imetapakaa katika idara mbalimbali kama vile afya,ujenzi,elimu,nishati,polisi hasa wale wa barabarani.

Sijawahi kusafiri nikakosa kuona rushwa inatolewa. Rushwa inaelekea kua kama kodi barabarani,kwa trafiki rushwa sio mada ngeni.

Wapo baadhi ya wafanyakazi wasio wazalendo,wasio jielewa,wenye tamaa ya hela,wasiokua na aibu,wasiokua na maadili na kila aina ya tabia mbaya kazini ambao hujiunga na magenge ya wenye hela na watoa rushwa. Wanajiunga nao kwa kuwanasua hata inapowekwa mitego wanawapa taarifa walengwa.

Kwa baadhi ya maeneo ukiaikia mtu amekamatwa na rushwa ujue huyo ni mkaidi dhidi ya makubaliano aliyopewa na watumishi wasio waadilifu au hana mtandao ndani ya ofisi hizo.

Kwa maeneo ambayo wanamaliza miezi sita bila kuisaidia serikali ingekua vizuri wakapumzishwa kwani wanaenda kinyume na malengo ya taasisi hiyo
 
Mkuu acha kupaniki hao ni watumishi wa umma wenye mikataba ya kudumu/permanent and pensionable.
Sasa ukija na hoja yako isiyokuwa na mashiko kisheria labda uwashauri wakenya waitumie
 
Ilitakiwa ifanyike tathmini ya jumla kwa zile ofisi ambazo hasiisaidii serikali kupambana na rushwa basi walengwa waondoke ili wapishe wengine. Kwanamna dunia ilivyo haiwezekani inaisha miezi sita ofisi haijakamata mlarushwa wala mtoa rushwa.
Ati wanasubiri wapelekewe malalamiko tena kwa kujaza fomu maalumu ndipo waje kumkamata mla rushwa, fikiria umekutana na traffic police anataka rushwa kisa ume over speed, uende PCCB, jaza fomu halafu waje kumkamata, sijui utamkuta bado anakusubiri hapo!!! muda mwingine huyo mlarushwa mwenyewe wanakunywa naye pombe samakisamaki
 
Ningekua Takukuru ningeamua siku nachukua basi tupu kutoka Mbeya hadi Dsm. Kila kituo namtanguliza konda na misimbazi ya moto,kisha nawakamata kiulaini.
Polisi wetu hawa nirahisi sana kuwanasa maana hata ukimwambia hapa sina hela twende ATM nikakutolee hela anashangilia kimoyomoyo mnaenda. Bado rushwa ipo na inazidi kushamiri kwani qanaoiendekeza niwale wanaotakiwa kuisimamia
 
Kwahiyo unashauri Kila gari liwe na afisa wa pccb?au unashauri Nini?NINI KIFANYIKE
 
Ningekua Takukuru ningeamua siku nachukua basi tupu kutoka Mbeya hadi Dsm. Kila kituo namtanguliza konda na misimbazi ya moto,kisha nawakamata kiulaini.
Polisi wetu hawa nirahisi sana kuwanasa maana hata ukimwambia hapa sina hela twende ATM nikakutolee hela anashangilia kimoyomoyo mnaenda. Bado rushwa ipo na inazidi kushamiri kwani qanaoiendekeza niwale wanaotakiwa kuisimamia
Kwahiyo unadhan kirahisi hivyo?ELIMU YA RUSHWA ITABIDI IANZIE KWAKO MKUU...[emoji3][emoji3]
 
Rushwa ni suala mtambuka, si kitu rahisi kuimaliza, labda kupunguza tu! Watoaji na wapokeaji wana tricks nyingi sana, pia kumbuka suala la ushahidi kwenye kesi ilivo ngumu.
 
Back
Top Bottom