Mtazamo wangu: Kuishi Sinza kunaweza kukuharibia maisha

Jamani mtu ka amua ku share story yake huwezi kumpangia au kum force kueni na uvumilivu sawa

Punguzeni kumpopoa😊
 
MUENDELEZO SEHEMU YA PILI

SAMAHANI KWA KUCHELEWA NILIUMWA SANA KICHWA LEO



Nikafika Salama Kwa Sister Nilikaa Mwezi Mmoja Bila Kutafuta mchongo wowote Nasoma Ramani

Sehemu ya 2..

Maisha ya Dar Es salaam Maeneo ya Temeke uporaji vichochoroni,Nilishihudia baadhi ya Matukio ingali Hayakuwa Mageni kwangu kwani nilishawahi Kaa Dar Es salaam Kitambo kwa Muda Mfupi

Sina Mchongo Nifanyaje Naishi Kwa Dada ingali si Dada Yangu Wa Damu Lakini Maisha Yanaenda Vizuri
Naanzia Wapi Hapa Sina Mtu Nayejuana Nae Ambaye Anaweza Nisaidia Naowajua Wote Hawawezi Nisaidia wameshindwa Saidia Ndungu zao Wa Karibu Kuwapa Michongo ya Maana Watanisaidia Mimi.
Nipambanae Huu ndo wakati wangu Wa Kuteseka Nisitie Huruma nilijisemea,Mwili wa Kubeba Zege Sina kilo zangu Hamsini kamili,Kimwili changu kubeba Zege Nitaendelea Kudumaa Nitumie Akili Mjini Hapa Nilijisemea.

Basi ikifika Jion nakaa Nje Naangalia Mazingira kitu kilichokuwa Kinanipa Furaha Kidogo Ni Kidemu changu cha kilichokuwa Kinaishi Morroco(Si Nchi, Morocco Hii ya Daslam) Nilikipata Hata Kabla Ya Kuja Dar es salaam Nilikuwa Najuana Naye Back Miaka Michache iliyopita ila Tumeanza Uhusiano una Kama Mwaka mmoja,Mahusiano Ya mbali yeye Dar Mimi Niko zangu Mkoani Tunadate 😃 Fimbo ya mbali Ndo Huuwa Nyoka Ya Karibu Atarukia akung'ate 😃.Ingali kuna Muda nilikuwa naona Kama ananiipotezea Focus Maana Bila Pesa Atakuacha Ninaamini katika Mapenzi na Pesa Na Mapenzi ya Pesa.

Hapo Nipo na Laptop yangu na Kisimu changu cha Samsung Cha zamani kina Buttons Pia Kina touch Kwenye Screen nilikuwa Nina Iphone Ila Niliiuza Nipate Pesa Inikimu Nikiwa dar Es salaam.
Laptop Nilinunua Kwa Pesa za Kudunduliza Nilizokuwa Napewa za kula shule Sikuwa Nakula Shule ingali mama Aliniongezea Kidogo Kipindi Niko Form 2 Nikanunua Laptop Ila Iphone Nilinunua Baada Ya Kumaliza Form 4 kwa Pesa pia za Kudunduliza kuna Mchongo Niliupata Nikaupiga kwa Miez Michache Nilipomaliza Form 4.
Nikauza Iphone Yangu kipindi Nakuja Dar nilikuwa Na Kisamsung Cha Kitambo ya Button pia Kinatouch Ndo Nilichokuwa Natumia pia Nakitumia Kama nikata Kuaccess Internet Kwenye Laptop Nafungua Hotspot Ila Whatsapp Hakikubal kwa sababu Ni Old Model.

Siku Moja nimefungua Laptop Niko napita Pita Mtandaoni Nikaona Kuna Mashindano Ya Kutengeneza Beats unatumiwa Vocal Unatengeza Beat Then Mshindi Anapewa pesa mwenye Beat Kali.
Hii Naiweza Ngoja Nijaribu bahati Yangu Ingali yalikuwa Ni ya Mtandaoni ila Udahili Ulifanyika Mikocheni(Kitu kilikuwa Ni Kigeni kwa Tanzania wachache sana Tulishiriki ingali kuna Mashindano Mengine Yalishawahi Kufanyika Wadhamini walikuwa Ni Maproducer wa Tanzania Mashindano Yalikuwa Yanajulikana Kama BeatArena hayo Ni Hivi karibuni yalioneshwa Channel 10 Kama Sikosei Ila Yangu Niliyofanya yalikuwa Ni ya watu wa Kutoka Nje )
Unapewa Vocal Then Unapewa muda Studio Ukisha Muda Unawasilisha kazi.
Nikashiriki Nikaangukia Pua Sikuweza Endelea Hatua inayofuata Lakini Hayo Mashindano Yalinipa Faida Niliweza Onana Na Vijana Wezangu Tukabadilishana Number.

Hapa Ndo Ukawa Mwanzo wa Mapambano nawaganda Hawa Niliokutana Nao Huku wanipe ramani wao Mjini Kitambo.
Baada ya Kama wiki baada ya Mashindano Kuisha Nilimpigia Simu jamaa mmoja ambaye nilishiriki naye kwenye Mashindano anaitwa Noel producer

Mimi "Inakuwaje Mkubwa"

Noel "Poa ni vp"

Mimi "Fresh"

Noel " Nambie kaka"

"Mimi" Kaka Unanikumbuka Tulikutana Mikocheni Kwenye Mashidano tukabadilishana Namba"

Noel "Nilibadilishana Namba Na watu wawil watatu sijakupata"

Mimi "Yule dogo white"

Noel "Oooh Vp mwanangu wanasemaje"
Mimi " Fresh tu,sasa Kaka Una studio Niibuke nichek chek mazingira Kujifunza Nini Mi bigina Kaka ninyi atleast"

Noel "Yeah kaka Ninayo Nimewekwa Hapa Ndo Huwa Napiga Vimeo Vyangu siku zinaenda"

Mimi "Lini Niibuke"

Noel " We Njoo tu Muda wowote tu mimi Nipo"

Mimi "Poa kaka Nitakuja Kesho Nipe direction"

Noel "Studio Ipo Mabibo Hapa"

Mimi "Poa kaka kesho Basi Tutasomana"

Basi Pakakucha Nipalangana Na Daladala mpaka Mabibo Nikafika akanielekeza Mpaka Studio Nikaingia akanikaribisha Maongezi Ya Kawaida yakaendelea Kujuana Zaidi

"Noel" Unapiga kinanda"

Mimi "Hapana Kaka Mimi Nachora tu"

Noel "Ooh Kinanda Muhimu kaka"

Ghafla Kaingia Jamaa

"Noel" Huyu Msanii wangu ila Huwa anajipigia Beat Mwenyewe Hahaa Mimi namalizia Vilivvyobaki narekebisha Rekebisha"

Mimi "Ni Vizuri Kuwa msanii Ila Una Idea ya Kupiga beat Pia Hata Kama Ni Kidogo"

"Noel" Kashafanya Vihit hit Huko kwao Tanga Ni maarufu Kidogo kwenye Miziki ile ya kibao kata,Baikoko wanamjua jua Huko kwao cheki youtube yake kama Unaweza Subscribe Umsupport"

Siku Ikapita Jioni nikarud Nyumbani hapo Nilikuwa Nishahama Kwa sister Naishi Pengine tu.Nikawa Naenda Studio Mabibo mara Moja Moja Naforce Kwenda Kila mara Ila Braza Ni kama Ananikataa Tena Kwa sababu Naenda sana Mimi Nikajiongeza Nikaacha Kwenda Nikaanza Angalia Chimbo lingine la Kwenda

Siku moja Nikapokea Simu Kutoka Kwa Homeboy Issa

Issa "Kaka Issa Hapa"

Mimi "Vp Kaka:
Issa "Fureshii Oyaa Kaka Vp Ramani Ya Mziki Umeisoma Tayari Huko"

Huyu Issa Alikuwa anaimba imba pia Alikuwa anasherehesha Maharusi kwa Kuimba Huko Mkoani kwangu Nilipotoka wanampoza kidogo anaishi"

Mimi "Bado Kaka Sio Poa Huku"

Issa "Sasa Kuna Braza flani Hv sijui utakuwa Unamkumbuka alikuwa mbele yetu madarasa tulisoma Nae shule ya Msingi kwa sasa na Yeye yupo Huko anaweza Kukupa ramani Kidogo Ingali yeye sio Mtu wa Mziiki Mziki Ila anajuana Na jamaa Mmoja hivi ni Producer na Ashafanya Hits Baadhi so anajuana Nae Anaweza Kukuunganisha Nae Alafu uzuri Pia huyo jamaa ni mwanae alfu Pia Wote Mahomboi "

Akanielekeza Nikawakumbuka Wote, Mabraza nikawakumbuka Kwa sura baada ya Kurushiwa Picha zao
Akanirushia Namba Zake Nimtafute Ashampanga Kila Kitu Nikamtafuta tukaongea Braza Akaniambia Anaweza Niunganisha Nae ila Jamaa kidogo ana vimba Siku Hizi kwa sababu anaball na Wasanii Wakubwa anafikiri maisha ndo Yameisha Kumbe Ndo mwanzo au Sa Ingine haringi Ila Yuko Busy Tu anajitafuta Ila Ni mzito Kukushika Mkono kwa sababu na Yeye bado anajitafuta Ila akaniambia ataniunganisha Na Jamaa Mwingine Hana Noma alfu ana Studio ya Kwake Kabisa ila Ana Michongo Mingine Anafanya Studio kaweka Tu kwa Vile anapenda Mziki kwa hyo hategemei mziki ili ale hawezi Kunja Ni Mtu safi kabisa

ITAENDELEA......
Mnivumilie mimi Sio Muandishi Mzuri sana Ila Najitahid kuandika So Nitakuwa naandika Nusu nusu kwa kwa Wale watu wanaandika Negative Kuhusu Huu Uzi unaweza unausubscribe Ukafatilia Nyuzi nyingine ruksa
 
Acha kutisha watu, nimeishi Sinza hakuna kilichonibadilisha ktk mipango ya maisha mpaka naamua kuondoka Dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…