Mtazamo wangu kwa Kennedytheremedy wa clouds fm

Ferrenga

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2016
Posts
942
Reaction score
1,658
Nawasalimu wana jukwaa wenzangu


Nimekuwa nikifwatilia industry hii ya media kwenye maswala yote yakiwemo ya michezo,muziki,na siasa pia.Leo nataka nimzungumzie huyu kijana kennedy ambaye anatangaza XXL ya clouds fm akiwa na Bdozen,Mchomvu na Mami,pia anakipindi kila jumamosi kinachoitwa bongo fleva..

Kwa kuanza kabisa,huyu kennedy alikuja clouds alitokea East africa redio ambako alikuwa anakipindi ambacho kilikuwa kina mvuto wa aina yake kilichokuwa kinaitwa the cruise na kipindi hicho alikuwa akihost na george bantu

Baada ya kuhamia clouds alianza na kipindi cha so so fresh kilichokuwa kimeachwa wazi na fetty,kilikuwa kinaruka kila ijumaa saa nne usiku..Baada ya fetty kuaga rasmi,kennedy alitambulishwa kama member mpya wa XXL na pia alipewa kipindi cha bongo fleva ambacho kinaruka kila jumamosi na kabla ya hapo kipindi hiki kilikuwa kinahostiwa na adamu mchomvu

Kijana huyu anakipaji kizuri sana cha utangazaji na kama mnavojua ipp media wamekuwa wakitengeneza presenter wazuri sana refer kina millard ayo na wengine..Kinachonishangaza ni yeye baada ya kufika tu clouds amerelax as if kila kitu amechamaliza kwenye tasnia yake ya utangazaji...kuwa clouds naamini ni njia ya kuweka kufika mbali kwa presenter yoyote anayejua anafanya nini


Amepewa kipindi cha bongo fleva ambacho anakiendesha kwa kiwango ambacho mimi naona bado..ukitizama zamani kipindi hiki kiliweza kuwaibua wasanii kama godzilla,dogo janja,young dee na wengine wengi..Kipindi kimekosa mvuto ambao unastaili..

Kwa nafasi aliyopewa kennedy,ingempasa awe amekiboresha sana kipindi cha bongo fleva na kuacha kufanya tu kazi ilimradi(kwa mazoea).anatakiwa pia aboreshe the way ana interview someone..Nafasi uliyopewa wewe kennedy hakika kuna presenter wengi wanatamani wangeipata,ila wewe mimi naona hauitendei haki


Kama uliweza kufanya the cruise kuwa kipindi bora,unashwindwaje kufanya pia bongo fleva kiwe na mvuto..

Ningependa nikushauri,ubadilike uwe yule kennedytherenedy wa earadio tuliyemjua,boresha kipindi cha bongo fleva kiwe na mvuto na pia ukiwa kwenye XXL jaribu sometimes kuwa critical kwenye maswala ya msingi..Bdozen niamini pia ni presenter mzuri sana kuwahi kutokea hapa bongo,kwahiyo unaweza kijifunza kidogo kutoka kwake

Ni hayo tu kwa sasa kwako wewe Kennedy...Naamini utaufanyia kazi ushauri wangu.
 
Ushauri mzuri ila shida moja WANAJUA WAKIFIKA CLOUDS ndio kila kitu amemaliza kwa hiyo anarelax na kufanya kazi kwa mazoea kama ulivyosema
 
ndoto yake kubwa ilikua ni kufika CMG siku moja,sasa imetimia hana malengo mengine ndomana yupo hivyo alivyo...
kwake ye CMG ni kama BBC
Acha kumlisha maneno..nimewahi Fanya nae kazi mahali Fulani kwa miaka miwili..na wala si kweli ulichokiandika..yeye ni mpambanaji na msaka tonge kama walivyo vijana wengine..ila azingatie ushauri..too bad haingii humu (namjua!) ila ataupata ujumbe!
 
Pale CMG kuna jamaa flani hiv ana bidii sana naamini atafika mbali..[HASHTAG]#Perfect[/HASHTAG] Crispin
 
Ngoja tu arelax hajui kama wenzake wakina jr junior, king smash... Wana zitamani hizo chance
 
Pale CMG kuna jamaa flani hiv ana bidii sana naamini atafika mbali..[HASHTAG]#Perfect[/HASHTAG] Crispin
sijaona bidii yoyote aliyonayo...zaid ya kila kukicha nikiona anaporomoka tofaut na alivyoanza!...kipindi kile cha CLUB 10 na weewe
 
Huyo Kennedy hayupo comfortable pale na ana kama kauoga uoga flani hivi hajiachii yani tofauti na alivyokuwa E.A Radio....labda ma-producer (kina Askofu)wa vipindi wanamkaba sana! hawampi script iliyonyooka......yani jamaa anaishia kucheka cheka tu...!
 
Acha kumlisha maneno..nimewahi Fanya nae kazi mahali Fulani kwa miaka miwili..na wala si kweli ulichokiandika..yeye ni mpambanaji na msaka tonge kama walivyo vijana wengine..ila azingatie ushauri..too bad haingii humu (namjua!) ila ataupata ujumbe!
presenter kama yeye haingii JF!!!!..anapata wapi info za moto..pia mshauri aingii huku jukwaani
 
Pale CMG kuna jamaa flani hiv ana bidii sana naamini atafika mbali..[HASHTAG]#Perfect[/HASHTAG] Crispin
Kweli perfect anajitahidi sana..japo kwenye XXL amepewa mda mchache tu kulinganisha na kennedy ambaye ni co-host wa bdozen
 
Ndo kitu ambacho hata mimi kinanishangaza..amwangalie mwenzake george bantu alivokifanya kipindi cha jahazi kiwe vizuri...
 
sijaona bidii yoyote aliyonayo...zaid ya kila kukicha nikiona anaporomoka tofaut na alivyoanza!...kipindi kile cha CLUB 10 na weewe
Hamna Perfect anafanya poa sana..sikiliza kipind chake cha On point kila jpili..jamaa anafanya vizur
 
Ushauri murua waache kufikiria CMG ndio mwisho wao,kuna BBC na mashirika mengine makubwa duniani kwanini asimwige mwenzake anold kayanda ambaye naye alikua anatangaza hapo lakini now yupo huko duniani? Waache kuridhika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…