Mtazamo Wangu: Tatizo la Simba SC kuwa na matokeo mabovu linaanzia hapa...

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Salaam..

Nimekaa nikajiuliza, hasa baada ya timu pendwa ya Simba Sc kuwa matokeo yasiyoridhisha kwa mechi za hivi karibuni baada, hii ni baada ya kuchapwa 0-3 na mwarabu, na jana usiku, kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam.

Tukiondoa sababu nyingine kama wachezaji kukosa nafasi za wazi, ambalo limeonekana kuwa tatizo kwa sasa pale Simba Sc, umri wa wachezaji na uchovu kwa kucheza mfululizo miaka mingi, lakini pia naona bado kuna tatizo jingine kubwa ambalo nalo hatujalitazama kwa umakini.

Nimekaa nikajiuliza, hivi ni ipi mantiki kwa Simba Sc, hasa viongozi wake, kuamua kuwa na makocha wawili, wote wenye sifa za kuifundisha timu, wenye umri mkubwa, kwa wakati mmoja?

Kama walishaamua kufuata maoni ya mashabiki kwamba Mgunda alikuwa hatoshi, wakaamua kumleta Mzungu, sasa ni sababu ipi inayowafanya waendelee kuwa na Mgunda pale kwenye benchi la ufundi?

Huu mkanganyiko unaojitokeza sasa matokeo yake ni kama vile Simba Sc imegawanyika makundi mawili, ina kocha wa viongozi, Mgunda, na kocha wa mashabiki waliotaka Mgunda aondoke kwa kura, mzungu.

Sijui ni kitu gani kinachowashinda viongozi wa Simba Sc kumwambia Mgunda asante kwa kazi yako, wamlipe chake, kisha aondoke, wamwambie ukweli sasa tumeamua kwenda na uelekeo tofauti, uwepo wake kwneye benchi naamini unawavuruga wachezaji kwa namna fulani.

Tumeona nyakati kadhaa Mgunda akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati mechi ikiendelea, huyu mtu anaweza kuwa anatoa malekezo tofauti na kocha mkuu anachotaka, matokeo yake ni kuwachanganya wachezaji, kwanini kocha mkuu asiachwe huru kufanya majukumu yake kwa nafasi?

Kwangu, viongozi wa Simba Sc ndio chanzo cha hili tatizo, kwani sijawahi kuona timu zinazojielewa hapa duniani zinakuwa na makocha wakuu wawili, hapa wanaajiri kocha mpya, na pale bado wanaendelea kubaki na yule wa mwanzo!, halafu tunajitapa tunakwenda kimataifa, mataifa yapi hayo?!

Viongozi wa Simba Sc pamoja na Mo wabadilike, waachane na mambo ya kimazoea na uswahili mwingi kwenye uendeshaji wa timu, tusipoamka mapema itakuwa too late.
 
Kupanga ni kuchagua, kazi kwa viongozi wa Simba Sc kuamua, hasa wakati huu tukielekea kwenye mechi mbili ngumu, za kuamua msimu wetu dhidi ya Vipers ya Uganda, chochote nje ya ushindi kwenye mechi hizo mbili, msimu wetu ndio utaishia hapo, kwani huku kwenye ligi, baada ya matokeo ya jana, automatically hatuna chetu tena.

Simba iko out of form, hakuna morali ya wachezaji na mashabiki, wakati kwa watani, mambo ni opposite, morali na form vyote viko upande wao kwa sasa.
 
Nani alokwambia simba sc ina makocha wakuu wawili? Muache mgunda nae apate rikizi mkuu punguza roho mbaya.Mgunda yupo kama daktari jadi(mfano mzuri reverse ya juzi) ndiyo kazi ya mgunda,angalia chuma ile alovaa mkononi ndiyo utajua inaitwa vyuma chakavu
 
🤣🤣🤣
 
Rizki iko popote, sitaki kuwaza kimasikini halafu tuweke professionalism pembeni, tutazidi kujimaliza.
 
Msijichanganye na hii fomu mliyonayo mkaja mbarali(ihefu)...
Mtachagua nyie,muache point au tuwauwe.
Huko Ihefu tutakuja kucheza na wadogo zetu.
 
Mbona Yanga wana Makocha wawili wakubwa?
 
Mchezaiji Kama baleke hata kupiga vichwa hajui nafas za waz anapiga nje toka mech na horoya raja na Jana pia kwa Azam

Binafsi Sion tatizo la kocha n ubora wa wachezaji wetu upo chini Sana

Sawadogo .. haendan na mfumo


SHOMARI na zimbwe wamechoka Sana magol kwa Sasa yanapitia kwao japo mtabisha sana


Baleke. .. mshambuliaji machachari ila siyo hatar langoni fikiria mazembe hii iliyooza inaamua kumuachia mchezaj bas ujue Hilo n garasa zaid

Boko mzuri ila Hana nguvu ile Tena umri umemtupa mkono hawez shindana na vjana
 
Mbona Yanga wana Makocha wawili wakubwa?
Kama hawana muingiliano kwenye majukumu yao sioni tatizo, tatizo lake pale mnapowaruhusu mashabiki kutoa maoni yao, kwamba hawamtaki fulani, halafu mnatimiza walichotaka, ajabu mnaendelea kubaki na yule wasiyemuamini.
 
Haya uliyoandika hapa ni matatizo mengine ambayo nimeyaainisha pale mwanzo kwa uchache, lakini pia nikiri yapo, ila kwanza tuanze na ule mvurugano pale kwenye benchi la ufundi.
 
Kwan makocha wote si wanashauriana na kufanya kazi kwa pamoja? Au we huwaoni?. Mgunda hawez kuwapeleka kokote. Tatizo mmejiandaa kushinda kila siku.... Hili ndo la kutibiwa
 
Maoni yako ni zaidi ya ujinga,samahani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…