Mtazamo wangu wa CHADEMA baada ya uchaguzi

Mtazamo wangu wa CHADEMA baada ya uchaguzi

def_xcode

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,896
Reaction score
5,181
Kwa mtazamo wangu upepo ulivyo Mbowe ana nafasi ndogo ya kushinda na kama kweli anatembeza pesa na kukafanyika janja janja akashinda basi chama kitapasuka vipande vipande.

Pia haijalishi nani atashinda, kwa jinsi mambo yalivyo bado kutakuwa na mpasuko maana watu watabaki na vinyongo na wengine ambao wanajulikana huyu ni team ya fulani lazima wawekwe pembeni kwa sababu ya kutoaminiana.

Iwapo atashinda Lissu, napo hapa kuna utata. Lissu ashaweka msimamo wake kuwa no reform no elections.

Kwa mantiki hii ni kwamba kama CCM na serikali yake haitofanya mabadiliko hawatashiriki uchaguzi. Nadhani CCM ingependa hili lifanyike kwani haijali hata kama chadema haitoshiriki, ili mradi vyama vingine vishiriki.

Kama chadema haitoshiriki, ina maana CCM ili kuonyesha uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, inaweza kuvipatia vyama vingine ushindi wa wabunge mfano ACT, CUF n.k. Lengo ni kwamba ionekane bunge ni shirikishi, halafu ili kuvifanya vyama hivi viunge mkono serikali kuwa vilishiriki kama vyama pinzani na vikapata ushindi.

Pia vitapata ruzuku na kufanya chama chenye wabunge wengi kuwa ndicho chama kikuu cha upinzani nchini na si chadema tena.

Mwisho CHADEMA itakosa ruzuku, itapoteza status ya kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, na mwisho kabisa Lissu huenda akaanza kulaumiwa kwa kukiua chama maana expectations vs reality.

Mimi ni team Lissu ila nachoona CHADEMA ina mtihani mkubwa sana ambao huenda haijawahi kupata mtihani mkubwa kiasi hiki.

Haijalishi nani atashinda ila CHADEMA itapitia msukusuko na kama ikishinda msukosuko huo basi bila shaka itakuwa imara kuliko hapo awali ila sioni itawezaje kushinda msukosuko huo.
 
Back
Top Bottom