Petro Masunga
Member
- May 5, 2023
- 7
- 7
Mapungufu ya mtu, yanaonekana katika ubinadamu wake, kwa kile anacho kifanya, hata hivyo tuna uwezo wa kufanya yote, kuwa makamilifu bila ya kurudia makosa yoyote. Jifunze. Unapotaza mapungufu ya mtu, fanya bidii sana wewe kuyasawazisha mapungufu yake, na huu ndiyo uwajibikaji. Hivyo uwajibikaji unaanza kwa mtu binafsi, sio kwa ajili ya kazi au nini. Hivyo basi, tukiacha kutazama kioo, na tukawa sisi kama kioo ambacho kina faa kutazamwa, maana yake tutakuwa na machaguzi mawili tu, kuwajibika au kuwajibishwa. Kuna umuhimu wa Sisi, kuacha kutazama nani amefanya nini au falani kafanya nini. Bali sisi wenyewe tujitazame tumefanya nini, na mwelekeo wetu ni upi. Kuamka kwa kijana ni ushahidi wa taifa!
.#vijanatunaweza.
Asante
.#vijanatunaweza.
Asante
Upvote
3