mtazano wangu kuhusu kansa kuzidi kungezeka tanzania

pakamwam

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2013
Posts
516
Reaction score
654
ni ukweli usiopingika kuwa kansa zimekuwepo toka zamani hata kabla babu yangu hajazaliwa lakini kwa jinsi rekodi zinavyoonyesha kansa imekuwa ikongezeka sana miaka ya hivi karibuni. nimejaribu kusoma na kujiuliza sana nafikiri kwa nchi yetu haya ndio yanasababsha kuwe na ongezeko kubwa la kansa

1. tumeanza kuwa na utamaduni wa kuthamini vyakula vilivyohifadhiwa kwa muda mreefu tujua ni ustaarabu. hapa nazungumzia canned and packed foods huko supermarket. ni aibu sana kijana anayemiliki nyumba kushindwa kuwa na kuku mmoja na kabustani ka mboga. tunathamini haya mavyakula na kusahau kuwa chemikali zinawekwa kwenye vyakula hata wadudu hawazitakia kabisa. mtu nashidwa kununua matunda na kutengeneza juice yake sababu ya uvivu na ustaarabu. haya mambo nafikiri yamekuwa yakichangia sana kuleta haya makansa maana makemikali mengi yanayohifya vyakula yana shida kwenye mwili

2. maisha ya kifahari yaliyopitiliza. kwa watanzania wengi kitambi na unene ni sifa njema. kwa mimi kitambi na unene ni uzembe na ulafi na ni ugonjwa. mtu anayenenepa kupita kiasi kwa mimi hafai hata kupewa dada yangu maana inamaanisha haijijali wala kujitambua so hawezi kuilinda familia yake. kuna shida nyingi sana zinaletwa na ulafi au kunenepa kupita kiasi

2. tabia zetu waafrika na hasa watanzania zinatuweka kwenye hatari ya kupata kansa sana sana kansa zitokanazo na virus kama Epstein-Barr Virus,Human papillomaviruses, Human herpesvirus 8, Hepatitis B virus, HTL virus AND Hepatitis C virus. Ambao hawa virusi wanasababisha kansa nyingi kama Genital tumors, Squamous cell carcinomaOropharyngeal carcinoma,Nasopharyngeal carcinoma,Burkitt's lymphoma, Hodgkin's diseaseT cell lymphoma, liver cancer, karposi sarcoma, t cell cancer a mengine mengi
njia kuu za kupata hawa virusi ni kwa majimaji na kugusana nikimaanisha kujamiana, kupigana mabusi na kushirikiana damu au maji maji yanayotoka kwa mwili wamwingi.

kuna haja ya kubadilisha mfumo wa maisha mfano unakuta mtu sanasana vijana anakutembelea hujui kalala na nini then mnalala kitanda kimoja bila kujali kabisa.

pia tabia yetu ya kuwa na wanawake wengi kama sifa na wanaume wengi kwa upande wa wanawake kama sifa. hizi tabia huchangia sana kupata virusi na ubaya wa hivi virusi huwa viweza kuwepo mwilini mpaka unakufa na ukaendelea kuathiri wengine

tabia ya kujiamini wazima kwa sababu hakuna sehemu inayouma. nawashauri watu kupima angalau mara moja kwa mwaka

kwa mwanamke aliyefisha miaka 30 anashauriwa kupima kansa ya kizazi au pap smear angalau kila mwaka mara moja
 
Hata mimi hili swala nilishawahi kujiuliza. Niligundua ni life style na kwenda na wakati.Matumizi ya simu za mkono,microwaves na madawa ambao serikali haithibitishi.
Madawa kwenye vyakula na hata nyama za kuku na nguruwe huko mtaani watz wamekuwa wabaya. Pesa mbele uhai hata Wao wenywe baadae.

Kuna watu wanauza michicha inayomwagiliwa na maji kutoka muhimbili. Sasa hapo kuna uhai kweli?
 
Karibu jf lakini hii mada haipo jukwaa stahiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…