Mtego wa Mwindaji Ulipokamata Chui

Mtego wa Mwindaji Ulipokamata Chui

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MTEGO WA MWINDAJI ULIPOKAMATA CHUI

Bahati nzuri familia zote mbili za Bi Khadija Baramia na Captain Meki Abdallah Ali Kayaya zipo.

Meki ni mchanganyiko wa Wamanyema upande wa kiumeni na Wangazija kikeni kwake.

Uhasama wa Meki na Kaujore ulianza ndani jela.

Inasemekana Meki alipambana na watesaji ndani ya jela na hawakumweza kwani alikuwa hodari wa kupigana aliwaonyoosha.

Ndiyo hayo maneno ya Kaujore ya kumuwahi kumuua asije kuuliwa yeye.

Ndipo alipompiga risasi.

Jitu joga lisilo na ushujaa wowote alishindwa na Meki aliyekuwa kwenye minyororo mkononi hana hata fimbo.

Kitabuni kuna kisa kama hiki Ibrahim Hussein anaeleza Khamis Abdulla Ameir alipopigana na watesaji wenye marungu na akawahenyesha yeye akipigananao akiwa kafungwa minyororo.

Ibrahim Hussein kaona mapigano haya kwa macho yake akiwa selo dirishani juu anachungulia chini.

Anamuona Khamis Abdulla Ameir anavyopigana na watesaji wake.

Wote wanamuogopa wanamkimbia hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kumkabili uso kwa uso (uk.58).

Mijitu mioga.
Chui wa karatasi.

Kisa hiki Khamis Abdulla Ameir hakukieleza kwenye kitabu chake, "Maisha Yangu."

Sijui kwa nini.

1724182456877.jpeg
 
Back
Top Bottom