T Kaiza-Boshe
Member
- May 27, 2013
- 20
- 39
UTATOFAUTISHAJE ASALI MBICHI NA ILIYOCHEMSHWA?
Unaponunua asali, ni muhimu kutofautisha asali mbichi na iliyochemshwa. Kwa tulio wengi, hii ni kazi ngumu. Hivyo tunasikiliza analosema muuzaji. Hakika hii si njia sahihi ya kujihakikishia ubora na usalama wa bidhaa muhimu ya chakula.
Wamasai wa Longindo, Arusha, wamevumbua suluhu; ama tuseme, msaada. Hii inahusisha kufungasha asali na nyuki waliokufa. Lengo ni kuonesha kuwa asali iliyo kwenye chombo hicho haijachemshwa.
Kwa asili ya asali, kikemikali, asali inawezakuwa inawezakuwa haijaathirika. Na kwa hiyo inakuwa bado ni salama kwa matumizi ya binadamu.
Kwa bahati mbaya, kwa mtu anayeona nyuki waliokufa kwenye asali kwa mara ya kwanza, na bila kuwa ameambiwa sababu na hali halisi (nature) ya asali, inatoa picha mbaya. Inaonekana ni uchafu na kutokuwa salama; jambo ambalo ni kinyume na lengo la muuzaji.
Inakuwa mbaya zaidi kama utando huo juu ya asali unakuwa ni vipandevipande visivyoonekana kama nyuki, ama sehemu za nyuki zinazoeleweka. Hiki ndicho kilichonikuta mimi wiki jana. Na kwa kuzingatia wafanyabiashara wengine wasivyojali wateja, niliamua asali hiyo niirudishe kwa mwanamama nilikoinunua nibadilishiwe nipewe iliyo safi.
Tukio hili, na mengine kama hayo, liliniacha nikiwaza kuhusu wajibu na ufanisi wa Afisa Biashara, Afisa Afya, Afisa Viwango anayehusika na chakula TBS, na wa Wizara Ya Afya kwa ujumla; katika kumhakikishia mlaji ubora na usalama wa bidhaa za chakula nchini.
Niliwaza pia kama mfumo wa sasa wa usimamizi wa ubora na usalama wa bidhaa za chakula unakidhi matakwa ya ubora na usalama wa chakula. Kuna hali haijakaa sawa, na kuna haja ya kuiweka sawa.
Kutokana na tukio nililolisimulia na matukio mengine yaliyofanana, ningependa kushauri Serikali itazame upya mfumo wa kisheria na wa kitaasisi unaohusika na ubora na usalama wa chakula kwa lengo la kuwianisha mfumo wa kisheria na uzingatiaji, kuboresha uwezo wa utendaji kitaasisi na uratibu baina ya taasisi, pamoja na kuboresha shughuli za ukaguzi wa bidhaa za chakula.