Mteja tusiyemfahamu kasahau chaji yake ya gharama sana hapa kijiweni. Bado tunamtafakari

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Tuko Kijiweni muda huu hapa maskani

Kuna chaji ya simu ipo hapa mezani Ina rangi nyeupe tena ya gharama kubwa imeachwa na mteja mmoja aliyekuja mapema leo asubuhi

Hatujui kaisahau kwa bahati mbaya au la na pia hakuna amjuaye mtu huyu anatokea wapi

Waliomuona asubuhi wanasema ni mtulivu , alikunywa kikombe kimoja tu, hakuwa na stori na yeyote na alivaa mavazi ya Heshima yasiyo ya Kiserikali

Bado tunatafakari tuchukue hatua gani na hivyo tumeona ni hekima kuomba mtushauri Ndugu zetu wa JF

Chaji hiyo nyeupe bado ipo mezani na hakuna aliyeigusa
 
Sasa sisi tuwashauri mumpigie wakati mawasiliano yake hamnayo?
Itunzeni akija mpeni
 
Mavazi ya kiserikali ni yapi mkuu
 
Kama ni hapo kijiwe cha kahawa niliisahau mimi,nitunzie itaifuata baadae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…