Mteja wa ajabu mwenye siri nzito

Mteja wa ajabu mwenye siri nzito

trojan92

Member
Joined
May 18, 2024
Posts
91
Reaction score
276
Hadithi ya kuvutia sana. Soma mpaka mwisho, utajifunza kutunza siri.

Siku moja Mwanaume mmoja mtanashati sana aliingia hotelini na akaomba kumuona bosi. Bosi alipokuja, hadithi ikaanza.

Mteja: Je, chumba namba 39 kiko wazi?
Bosi: Ndiyo, bwana.
Mteja: Naweza kukiomba?
Bosi: Bila shaka unaweza.
Mteja: Asante.

Kabla ya kwenda chumbani, mteja alimwomba bosi ampe kisu cheusi, uzi mweupe wa sentimita 39 na chungwa lenye uzito wa gramu 73. Bosi alikubali ingawa alishangazwa na vitu vya ajabu ambavyo mteja aliomba kuwa navyo katika chumba chake. Mteja aliingia chumbani, hakuomba chakula wala kitu kingine chochote.

Kwa bahati mbaya, chumba cha bosi yule bosi kilikuwa karibu na chumba namba 39. Baadaye usiku wa manane, bosi alisikia sauti za ajabu na kelele chumbani mwa mteja huyo. Sauti za wanyama wa porini na za vyombo na sahani zikidondoshwa sakafuni.

Bosi hakulala usiku huo. Aliendelea kufikiria na kujiuliza nini kinaweza kuwa chanzo cha kelele hizo katika chumba cha mteja yule. Asubuhi, mteja aliporudisha funguo kwa bosi, bosi hakutaka kupokea funguo aliomba kuona chumba kwanza.

Alienda chumbani na kukuta kila kitu kikiwa sawa. Hakuna kitu cha ajabu. Aliukuta hata uzi, kisu cheusi na chungwa mezani, vyote vikiwa havijatumika.

Mteja alilipa bili na akawapa wahudumu wa hoteli fedha kama sehemu ya asante kwa huduma nzuri na na akaondoka hotelini akitabasamu. Bosi alikuwa na mshtuko lakini hakuweza kusema alichosikia kwa wahudumu wa hoteli. Kwa kweli, alianza kujishuku mwenyewe.

Baada ya mwaka mmoja, mteja yule yule alijitokeza tena. Aliomba kumuona bosi tena. Bosi alikuwa kwenye kitendawili. Akiwaza itakuwaje? Mteja aliomba vitu vile vile: chumba namba 39, kisu cheusi, uzi mweupe wa sentimita 39 na chungwa lenye uzito wa gramu 79.

Safari hii, bosi alitaka kujua ukweli kwa njia zote zinazowezekana. Alikesha usiku mzima, akisubiri kitu kutokea. Baada ya usiku wa manane kuwadia, sauti na kelele zile zile zilianza, safari hii zikiwa kubwa na hazieleweki kuliko mwaka uliopita. Bosi aliogopa sana.

Asubuhi kulivyokucha, kabla ya kuondoka, mteja alilipa bili yake na akaacha fedha kubwa mezani kwa wahudumu wa hoteli kama sehemu ya asante kwa huduma nzuri. Aliondoka huku Tabasamu likichanua katika uso wake.

Bosi alianza kutafuta maana ya kila kitu ambacho mteja aliomba kuwa nacho. Kwa nini aliomba chumba namba 39? Kwa nini uzi mweupe? Kwa nini kisu cheusi??? Kwa kweli, bosi hakupata jibu la kuridhisha kwa maswali haya yote!

Bosi sasa alikuwa akisubiri kwa hamu mwezi wa Machi, mwezi ambao mteja huyu alijitokeza. Bosi alimuona mteja huyu kama mtu wa ajabu.

Bosi kwa mshangao, siku ya kwanza ya Machi, mteja yule yule alijitokeza. Aliomba vitu vile vile. Alitaka kuweka chumba kile kile, alitaka kuwa na vitu vile vile kama zamani. Kama kawaida usiku ulivyowadia, Bosi alisikia kelele zile zile, safari hii zikiwa kubwa zaidi kuliko miaka ya awali.

Asubuhi, mteja yule wa ajabu alipokuwa anaondoka hotelini, bosi alijitahidi kumsihi mteja na kumuomba ajue siri ya kelele hizo chumbani.

Mteja - ''Kama nitakueleza siri, unaahidi kutomwambia mtu yeyote?''
Bosi- ''Naahidi sitamwambia mtu yeyote''
Mteja - '' Tafadhali Apa''
Bosi - ''Naapa sitafichua siri yako''
Hatimaye, mteja alifichua siri yake kwa bosi.

Kwa bahati mbaya, bosi alikuwa mtu mwaminifu. Hadi sasa hajaeleza siri yake kwa mtu yeyote. Atakapofanya hivyo, nitakujulisha asante kwa kusoma.

Unaachaje kushare stori hii kwa wengine ili wajifunze wafurahi na wajue umuhimu wa kutunza siri
 
Back
Top Bottom