Mtendaji Katavi aliyeomba Rushwa ya 200,000 ahukumiwa miaka mitano jela

Mtendaji Katavi aliyeomba Rushwa ya 200,000 ahukumiwa miaka mitano jela

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi imetoa hukumu katika Shauri la Jinai Na. CC. 72/2021 dhidi ya Florence Noel Malilo (Kaimu Afisa Mtendaji Kijiji cha Mapili, Halmashauri ya Wilaya Mlele).

Mshtakiwa alishtakiwa kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa ya shs. 200,000.

Katika kesi hiyo iliyosikilizwa na Hakimu Mkazi, Bilal Mohamed, mshtakiwa amekutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Tsh. 1,000,000/= ambapo mshitakiwa amelipa faini na kuepuka kifungo.
 
Basil Mramba marehemu sikumbuki alipewagwa adhabu gani, lakini ukiangalia hasara na ubadhirifu waliofanya umeua kwa njaa na maradhi watanzania wengi sana kwa mamilioni..
 
Basil Mramba marehemu sikumbuki alipewagwa adhabu gani, lakini ukiangalia hasara na ubadhirifu waliofanya umeua kwa njaa na maradhi watanzania wengi sana kwa mamilioni..
Haya mashetani yanayoiba huku yamevaa suti hayaguswi na mtu
 
Basil Mramba marehemu sikumbuki alipewagwa adhabu gani, lakini ukiangalia hasara na ubadhirifu waliofanya umeua kwa njaa na maradhi watanzania wengi sana kwa mamilioni..
Ahhhh, mzee alipewa adhabu ya kufagia hospitali tu
 
Back
Top Bottom