Yatima hadeki ndiposa najiuliza Watetezi wa Wamachinga ni nani?
Ni kile Chama cha Wakulima na Wafanyakazi ( CCM ) au ni hiki Chama cha Wafanyabiashara ( Chadema )?
Kwani kura walimpa nani?
CCM sio chama cha wakulima wala wafanyakazi tena
Wakati huo kilipoanzishwa kulikuwa wafanyabiashara wengi wenye asili ya Kihindi, Wahindi wao walikuwa daraja la pili toka kwa mkoloni mzungu
Leo hii wafanyabiashara weusi ni wengi sana
Kwa sasa CCM sio chama cha siasa bali ni Serikali inayosubiri kuapishwa kila baada ya miaka mitano.
CCM ni kivuli tu kuhalarisha vyama vingi, Kiuhalisia CCM ndio Serikali
CCM ilishashinda kabla hata ya uchaguzi penda au usipende
Kama kuna kuwa na Fair play na uwanja sawa wa mapambano mikoa kama Dar, Mbeya au Arusha ccm haiwezi kuchomoka
CCM sio chama cha wakulima wala wafanyakazi kwa sasa CCM ni Serikali kamili iliyojificha nyuma ya demokrasia za uchaguzi na vyama vingi, Labda katiba ibadilike na ccm ianze upya na ruzuku zitolewe kwa usawa
Kwa hali hii na kwa njaa hizi na matumbo Haya yetu yana njaa, Tegemea kila mwaka ccm kushinda
Kila mtu anataka pesa na maisha safi,
Thubutu, Nani anataka kila wakati mara TRA mara uhujumu Uchumi, Ni lazima uunge mkono juhudi za kila mwenyekiti