Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za wakati huu?
Kuna mambo mengi sana ambayo mtu anaweza kuyafanya katika maisha yake hapa duniani, lakini hata kama utayafanya yote ila usipofanya jambo moja tu basi hakuna umuhimu wa wewe kuwepo duniani.
JAMBO LA MUHIMU KULIKO LOTE NI KUHAKIKISHA KWAMBA KATIKA MAISHA YAKO HAPA DUNIANI UNAOTESHA ANGALAU MTI MMOJA. UKIWEZA OTESHA HATA ZAIDI.
Leo nataka nizungumzie kuhusu upandaji wa miti katika mtazamo wa kijasiriamali na faida zake katika mafanikio yako.
Katika kulizungumzia hilo nataka nieleze kabisa kwamba, nimetumia neno kupanda kwa sababu ya utata wa neno hili. Kupanda kunaweza kumaanisha kukwea au kuotesha.
Ninapozungumzia mti wa mtunda namaanisha maana zote mbili na ninapozungumzia mti wa kivuli nazungumzia maana ya kuotesha.
Miti ya kivuli na matunda ni zile fursa, watu, vitu au mambo ambayo unayafanya ambayo hutarajii yakupe matokeo ya wakati huo lakini kwa hakika ukiyatunza na kuyafanya vyema yatakupa matokeo mazuri sana.
Kutegemea na hali yako ya maisha unaweza ukawa unahitaji miti ya matunda tu au miti ya kivuli au yote kwa pamoja na unaweza kuitajika kuikwea tu au kuiotesha na kuikwea pia.
Ni kwa vipi unaweza kupanda miti ya matunda?
Kupanda miti ya matunda ni kuwekeza na kuwa na bidii. Unaweza kuwekeza katika elimu na ujuzi wako, unaweza kuwekeza katika biashara, unaweza kuwekeza katika rasilimali kama ardhi, nyumba etc, unaweza kuwekeza katika watu kwa kuwatendea wema na kuwasaidia na kuwapa fursa.
Matunda haya yakikomaa unaweza kuyachuma na kuyala wakati wowote unapohitaji kwani yatakufaa wakati wowote wa dhiki na wa faraja.
Ni kwa vipi unaweza kupanda miti ya kivuli?
Mti wa kivuli unapandwa kwa njia moja tu nayo ni kwa kuweka akiba, ndio kwa kuweka akiba ya kutosha unaweza kujijengea usalama katika nyakati fulani na hata ukapata muda wa kupumzika. Hivyo basi jifunze kuweka akiba.
NImalize kwa kusema tu kwamba kwa mwaka 2020 basi tujitahidi kupanda miti. Miti ya kimazingira, miti ya kijamii, miti kielimu na hata miti ya kiuchumi.