Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Inasadikika miti hii inafuga mashetani, kule Benini sadaka hutolewa chini ya mti huu hasa kwa wenye matatizo ya uzazi.
Unaweza kurefuka kufikia mita 50 au futi 160. Maajabu ya mti huu huwa miwili jike na dume pamoja. Dume hutoa mbelewe zinazojifunga kwenye majani ya jike. Jike hutoa maua kati ya mwezi December na January. Baada ya maua hutoa jamii ya nuts zinazopendwa kuliwa na nguchiro, popo au ndege. Hawa ndiyo wasambazaji wakuu wa mbegu za mvule.
Kutokana na ubora wa mbao ndiyo nilifuatilia uwezekano wa kuotesha mitii shambani kwangu. Katika utafiti niliyo ufanya, mbegu zinazoweza kuota ni zile zilizopita tumboni mwa viumbe nilivyo vitaja hapo juu. Mvule ukiwa mchanga haupendi mwanga wa jua na unapenda unyevu nyevu.
Baada ya kipindi cha uchanga kuisha Mvule unaweza kustahilimili ukame mradi mizizi yake ifikie maji chini ya ardhi. Ndiyo maana inastawi katika misitu ya pwani kwenye high water table.
Miti hii ipo hatarini kupotea duniani na ni moja ya miti inayohifadhiwa na UNESCO