Mkuu wa wilaya ya Gairo, mwanamama Siriel Mchombe, Jumapili iliyopita alishangaza waumini wa Kanisa la Assemblies of God, kwa Samson, Gairo kufuatia kutoa maneno yenye kuashiria kumpigia debe mtia nia wa Jimbo la Gairo kwa tiketi ya CCM, Joel Mmasa.
Baada ya ibada kumalizika, baadhi ya waumini walisikika wakisema kuwa, DC huyo anataka kulifanya kanisa hilo kuwa jukwaa la siasa.
Hilo limetokea huku kukiwa na shutuma nyingine kuwa, baada ya Joel kutia nia kwa kuchukua fomu na kurejesha akitaka ubunge wa jimbo hilo, aliitwa kwenda kutoa mahindi gunia 9 kwenye shule moja ya msingi kitendo kilichochukuliwa kuwa, ni kuanza kampeni kabla ya muda na pia ni rushwa.
Baadhi ya viongozi Gairo, wanadai kuwa, DC huyo anaonekana kufanya juu chini ili kuhakikisha, Joel anaingia bungeni mwaka huu kupitia jimbo la Gairo.
DC huyo anadaiwa kuwatumia watu watatu kumshusha mbunge Shabiby ambaye pia ametia nia kugombea mwaka huu. Watu hao ni mwalimu Aron, Luc Brighton na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CCM wilayani hapo, Omar Awadhi.
Huyo Awadhi, siku za karibuni alitoa mpya moja. Waziri wa Maji, Makame Mbarawa Mnyaa alitembelea Gairo kukagua miradi ya maji.
Alipomaliza hotuba, Awadhi aliomba kuuliza swali, Mbarawa akakataa, lakini DC huyo akalazimisha waziri akubali swali.
Waziri Mbarawa alimpa nafasi Awadhi, swali lake lilihusu mradi wa maji kukwama, akidai mbunge Shabiby kuhusika na kuchakachua pesa za mradi.
Mbarawa katika kujibu swali hilo, kwanza alimwambia muuliza swali kuwa, katika utawala wa Mheshimiwa Rais Magufuli hakuna mtu anayeweza kula pesa za mradi wowote, achilia mbali wa maji.
Pia waziri Mbarawa alimuuliza Awadhi kuwa, Shabiby amezilaje pesa za mradi wakati pesa inatoka serikalini zinaingia kwenye mradi na wasimamizi wapo!
Baada ya waziri kuondoka, baadhi ya watu walisema inaonekana swali la Awadhi lilikuwa na mkono wa DC huyo ndiyo maana alilazimisha waziri akubali swali.
Baadhi ya wananchi wilayani Gairo wamemtaka DC huyo kujikagua katika uongozi wake kwani amekuwa akilumbana lumbana sana na baadhi ya watendaji.
Aliwahi kukwanguana na mheshimiwa Shabiby mpaka rais Magufuli akaingilia kati. Lakini hivi karibuni pia amewahi kukwaruzana na madiwani wake kitendo kinachowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa, anajivuna kwa vile mumewe ni daktari mkubwa eneo fulani serikalini.