Uchaguzi 2020 Mtia nia Ubunge CCM ajitosa kukomboa jimbo la Arumeru Magharibi

Uchaguzi 2020 Mtia nia Ubunge CCM ajitosa kukomboa jimbo la Arumeru Magharibi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
MMOJA ya watia wa jimbo la Arumeru Magharibi, Ezekiel Elphas Mollel amejitosa kumuunga mkono mgombea mteule wa CCM, Noar Lembriss Mollel akidai ni operesheni kabambe ya kulikomboa jimbo hilo lililopo chini ya upinzani na kulirejesha CCM ambapo amewaomba wanaCCM pia kuwa wamoja katika kumwombea kura Rais John Magufuli.

Akiongea na vyombo vya habari Ezekiel ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliokuwa watiania 61 wa jimbo hilo amekipongeza chama cha mapinduzi kwa kumteua Noar Lembris akidai kwamba uamuzi huo unapaswa kuzingatiwa na wanaccm kwani zamu yake bado na kuwataka kumuunga mkono mgombea huyo.

Ezekiel amekuwa kada wakwanza kujitokeza hadharani kumuunga mkono mteuli huyo Lembris Noar ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha kupitia Chama cha Chadema kabla hajahamia CCM, akidai kuwa nia yake ya dhati ni kuona jimbo la Arumeru masharibi linatoka upinzani .

Ezekiel ambaye kitaaluma ni Mwalimu,amesema yupo tayari kusubiri wakati mwingine wa kuwania nafasi ya ubunge ila kwa sasa itoshe kusema kwamba nguvu yetu ni kukomboa jimbo letu la Arumeru Magharibi"

Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Chadema chini ya mbunge aliyemaliza muda wake Gibson Ole Meseiyeki ambaye amepata tena uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chadema .

IMG-20200822-WA0007.jpg
 
Hapo wangeungana wote 61 lakini wote watakalishwa chini
 
Huyu jamaa niliwahi kumuangalia kwenye mahojiano na Nyanda Star TV. Seriously nilidhani ana utindio wa ubongo. Yani ana bwabwaja sana. Ningeshangaa sana kama CCM wangempitisha. Jamaa kichwani ni empty aisee
 
Kitaaluma mwalimu!!! Hii fani wengi hawajitambui kabisa
 
Back
Top Bottom