Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Angejipa muda akawasikiliza hata wana ccm wenyewe angebaini kuwa chaguzi za Tanzania si huru na haki!Mwanachama Wa Chama Cha Demokasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye ni mtia nia wa Urais kupitia Chama hicho, Ndugu Romanus Mapunda, amejitokeza Hadharani na kupinga vikali sera ya " No reform No Election" Kwa Kuwa unaweza kuzima ndoto yake kuwa Rais na Haina Afya Katika Demokrasia ya Nchi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Mimi kama mwanachama Wa CHADEMA, najitokeza kupingana na mwenyekiti juu ya sera hii, Chadema tunapaswa kwenda kushindana kwenye uchaguzi wa Huru na wa haki"
Hajui asemalo, CHADEMA kuna demokrasia halisi CCM sasa, Yule Mzee wa Watu kafukuzwa uanachama kwa kukosoa Tu vile Samia amejitangaza mgombea bila kufuata utaratibu"Mimi kama mwanachama Wa CHADEMA, najitokeza kupingana na mwenyekiti juu ya sera hii, Chadema tunapaswa kwenda kushindana kwenye uchaguzi wa Huru na wa haki"
Hata kama wapo,, na wanaotaka kugombea je hawataenguliwa, je hawatatekwa, je wataweza kufanya kampeni? Je mawakala wao wataruhusiwa kusimamia uchaguzi? Je wakishinda watatangazwa, Je wanaCDM hawatafung,, guiwa kesi za kumbambikiwa kama 2020 zaidi ya wanachama 1000 waliwekwa mahabusu na wengine mpaka leo bado wapo ndani. CDM wakishiriki uchaguzi ktk mazingira haya hasara ni kubwa kuliko faida, kama wanaitaji kupata angalau karuzuku kakuwasogeza sogeza washiriki lakini wategemee hayo niliyoyasema, ujinga ni wakati wa kwenda si wakati wakurudi. Mimi nadhani vyama vile ambavyo vipo kwa ajili ya maslai ya viongozi wao binafsi vihiriki kwasababu watapata pesa, ila vyama vyenye malengo ya kuchukua dola wasishiriki huu uchaguzi wa maigizo wakomae mpaka katiba mpya ipatikane na tume huru, na watanzania wasizani swala hili linawahusu wazungu au wamarekani. Swala hili ni letu wenyewe hao wenzetu walipigania mambo haya siku nyingi ndiyo maana wanamaendeleo wala hawakusaidiwa na mtu yoyote ila kama sisi tunaona bado hatupo tayari basi tuendelee hivi hivi na mifumo yetu ya hovyo mpaka pale lasilimali xetu ztakapo kwisha nakuanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe. Tanzama shule za Serikali hakuna waalimu darasa moja watoto 200, Angalia hositali za uma Madaktari hakuna, Angalia mahakama, mahakimu na majaji ni wachche sana Kesi unaweza ukapangiwa kurudi baada ya miaka mitatu. Haya yote yanafanyika kwasababu viongozi waliopo madarakani hawawajibiki kwa wananchi na hawawajibiki kwa sababu hatujawachagua.Tutakapo pata viongozi ambao tumewaweka madarakani kwa matakwa yetu watatuhuduia kwasababu wanajua kuwa tutawawajibisha. Ila hawa wanajua uwa hatuna cha kuwafanya kwahiyo wanatuuruza tu kama Ng'lombe, utekaji unaendeleanchini watu wanatoweka lakini huoni mtu yoyote kushtuka kama vile uganda ya Idiamini na Maliyamungu. Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, hii itarudisha heshima na nidhamu ya viongozi kuwaheshimu wananchi wao wanaowapiga kura. Ila tukiacha hivi bora liende litaenda kweli.Lissu ni dikteta, anazuia wanachama wa chama chake kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchaguliwa.
Wanachadema wenye nia ya kugombea, wamtenge dikteta Lissu.