Mtibwa mabingwa Tusker

Babuji

Senior Member
Joined
Nov 27, 2008
Posts
197
Reaction score
4


OMARI Gumbo wa Mtibwa Sugar atakuwa na haki ya kukumbuka na Watanzania baada ya kufunga bao safi na la ushidni kwa njia ya penati katika dakika ya 60 na kuiwezesha timu yake kutwaa kombe la Tusker baada ya kuifunga Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) bao 1-0.

Penati iliyosababisha bao hilo ilitokana na beki wa URA, John Karangwa kumchezea vibaya Idrissa Rajabu aliyekuwa akichanja mbuga ndani ya eneo la hatari la timu hiyo kutoka Uganda.



Gumbo alipiga penati safi iliyomwacha kipa Abey Dhahiri, akiruka upande wa kulia na mpira kutinga wavuni upande wa kushoto. Katika mchezo huo, Mtibwa ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini ubutu wa washambauliaji wake uliioksesha mabao ya wazi hasa kipini cha kwanza

 



Habari kubwa sana hii. Tunashukuru kombe limebakia Tanzania.
 
Angalau Mtibwa wametutoa Watz kimasomaso!

Hivi Visiwani hakuna timu iliyoshiriki?
 
Hongera Mtibwa Sugar kwa kulibakiza Kombe nyumbani
 
Angalau Mtibwa wametutoa Watz kimasomaso!

Hivi Visiwani hakuna timu iliyoshiriki?

Visiwani hakuna timu iliyoshiriki...Nadhani sababu kubwa ni kwa sababu mashindano yanadhaminiwa na bia ya Tusker na visiwani hawaruhusu udhamini wa michezo unaolenga kutangaza vileo
 

Ongera Tanzania, Ongera Mtibwa kwa kututoa kimaso maso!
 
Visiwani hakuna timu iliyoshiriki...Nadhani sababu kubwa ni kwa sababu mashindano yanadhaminiwa na bia ya Tusker na visiwani hawaruhusu udhamini wa michezo unaolenga kutangaza vileo

Balantanda,
Ahsante mzee! Ila aslimia 30 ya pesa ya kodi ni vileo..na hata misaada toka Ulaya pia aslimia ya pombe ni kubwa!

heri kushiriki tu!! sasa bia sii ndo hujenga barabara? je unaweza kukataa kupita ktk barabara kwa vile imejengwa kwa bia?

Sorry ni out of topic kidogo!

Nami nawapongeza Mtibwa!
 

Hayo ndo mambo ya Zenji mkulu
 

ikiwa pesa nyingi inapatikana kwa madawa ya kulevya jee ndio tukubali kuwa ni sawa ?
 
ikiwa pesa nyingi inapatikana kwa madawa ya kulevya jee ndio tukubali kuwa ni sawa ?

Tofauti na biashara ya pombe, biashara ya madawa ya kulevya hairuhusiwi Duniani. Siyo legal business, kwa hiyo inaweza kuwapo popote pale, hata Saudia.
 
Hongera mtibwa kwa kubakiza kombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…